Msemaji wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli kuelekea kilele cha wiki ya Wananchi amewaita mashabiki wa Yanga wakaujaze uwanja lakini pia hakusita kujinasibu na kusema wana kikosi kilichosheheni.
Bumbuli pia alikua pamoja na msemaji wa klabu ya Aigle Noir na kusema wameshafika tayari wanatarajia kufanya mazoezi nao pamoja katika uwanja wa Benjamini Mkapa.
“Maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90 watu jana walishuka na Chopa kwenda kufanya “sound check” uwanja wa Taifa. Tutakwenda kuona uwanja jinsi maandilizi yalivyokamilika. Wageni wetu wamewasili jana, wamepata nafasi ya kupumzika na jana wamepata muda wa kufanya mazoezi pale katika uwanja wa Chuo cha Sheria.
Leo tutakua nao uwanja wa Benjamin Mkapa tutafanya nao mazoezi pale. Tutaanza sisi mazoezi kwa saa moja kuanzia saa kumi kamili mpaka saa kumi na moja jioni halafu wataingia wao mpaka saa kumi na mbili jioni.” Hassan Bumbuli
Nae msemaji wa Aigle Noir hakusita kujinasibu na kuahidi mchezo mzuri licha ya kua ni mchezo wa Kindugu tu huku aliahidi burudani kwa mashabiki.
“Tuna wachezaji wengi hata sisi pia, huyu (Bumbuli) amesema maneno mengi, hata sisi tuna wacheza kutoka Ivory Coast, Cameroon na wengine wanatoka hapahapa Tanzania pia. Tumejipanga vizuri tunajua ni mechi ya kirafiki mechi ya undugu lakini mechi lazima iwe nzuri, show iwe sawa kwa mashabiki.” Fabrice