Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Simba Ahmedy Ally amesema Ligi ya msimu huu inashirikisha timu dhaifu kutokana na aina ya msimamo ulivyo na timu shiriki zilivyo. Kupitia ukurasa wake wa instagram Ahmed Ally aliandika hayo.

“Katika timu 16, timu 14 zinaweza kushuka daraja, hii sio aina ya ligi tunayoihitaji haiwezekani timu nyingi zigombanie kushindwa,” Ahmed Ally

Msimamo Ligi Kuu ya NBC.

“Ligi yenye ushindani ni Ile ambayo timu nyingi zinagombania ubingwa. Timu nyingi Msimu huu zimekua dhaifu, tupo round ya 22 lakin ni timu tatu tu zimefikisha point 30+,” aliongeza

Ahmedy Ally pia alikiri Simba msimu huu ilikua dhaifu baada ya kushindwa kubeba alama tatu miongoni mwa timu dhaifu katika Ligi msimu huu.

Mohamed Hussein wa Simba dhidi ya Reliant Lusajo wa Namungo

“Msimu uliopita hadi kufika round ya 22 japo timu zilikua nyingi lakini timu 7 zilikua na points 30+. Hii ni hatari kwa sababu Bingwa anaweza kupatikana kwa kufunga waidhaifu wengi.” Ahmed Ally

“Najua utauliza kwanini na wewe usiwafunge hao dhaifu wengi Ili uwe Bingwa, ukweli ni kwamba katika hizo mechi zetu dhidi ya timu dhaifu nasi tulitanya udhaifu,” alisema Ahmedy msemaji wa klabu ya Simba.

Sambaza....