Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally amewatoa mashaka wapenzi na mashabiki wa klabu ya Simba wasiwasi kuhusu kiwango cha kiungo wao Ismael Sawadogo.

Ally amesema Sawadogo ni mchezaji mzuri shida tu kwamba bado hajazoea mazingira na anakosa utimamu wa mwili lakini si mchezaji mbovu kama wanavyosema.

 

Ahmed Ally “Sawadogo (Ismail) bado hajatupa kile tunachokihita Wanasimba kutokana na kushindwa kuwa fiti, bado hajazoea mazingira lakini pia bado hajazoeana na timu hivyo akishakua fiti atatusaidia sana.” 

Msemaji huyo wa klabu ya Simba ambae amesisitiza mashabiki kujaa kwa wingi katika mchezo dhidi ya Vipers amesema Sawadogo ni mchanganyiko wa viungo wa zamani wa Simba.

Ismail Sawadogo

“Sawadogo ni mchanganyiko wa wachezaj wengi ni mchanganyiko wa Fraga na Lwanga lakini pia zaidi ni ball player anakupa faida yakucheza mpira pia, ana uwezo mkubwa kwenye kupiga pasi na kuchezea mpira. Tumpe muda zaidi nakuhakikishia ule ni usajili mzuri na sahihi kwa Simba,” Ahmed Ally alisema.

Kumekuwepo kwa maneno kutoka kwa wapenzi wa kandanda mara kwa mara wakionyeshwa kutokuridhishwa na kiwango cha nyota huyo aliejiunga na Simba katika dirisha dogo akitokea kwao Burkina Faso alipokua mchezaji huru baada yakukaa nje mda mrefu kutokana na majeruhi.

Sambaza....