Sambaza....

Kama hapo awali tulivyokuwa tumetoa dokezo la kikao, vitu vichache tulikuwa tumepatia kwenye baadhi ya vitu.

Abdallah Saleh na Thomas Mselemu walikuwa katika makao makuu ya shirikisho la Soka Tanzania kwaajili mkutano huo.


    • Klabu ya Simba yaomba radhi kwa Shirikisho na Watanzania

Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amesema wao kama uongozi wa klabu hawajafurahishwa na kitendo cha wachezaji wao ya kushindwa kujiunga na kambi ya timu ya taifa inayojiandaa dhidi ya Uganda ya kufuzu AFCON

Vilevile amewaasa mashabiki wa klabu ya Simba waiunge mkono timu yao ya Taifa na kuweka Utaifa mbele wakati wa mchezo huo wa kufuzu dhidi ya Uganda utakaochezwa katika dimba la Nambolee, Kampla. “Mimi nitaongoza mashabiki katika uwanja wa Nambolee kuishangilia Taifa Stars, ili iweze kuibuka na ushindi katika mchezo huo muhimu” Manara.

Mashabiki wanaoishi mikoa ya karibu na Uganda hasa kanda ya Ziwa, waende kwa wingi Jijini Kampala kuisapoti timu yao, amesisitiza.

      • TFF na Klabu kufafanua nini kilitokea na nini kifanyike mbeleni.

    Kwa mujibu wa msemaji wa Simba, pande zote mbili ziligoma kuongelea zaidi kuhusu hili la kwanini wachezaji walishindwa kuripoti kwa wakati uliotakiwa. Wamekubaliana waangalie ya mbele tu.

    • Klabu ya Simba kuendelea na ratiba yake ya Ligi dhidi ya Lipuli FC.

Hakuna mabadiliko ya ratiba yoyote ya ligi kuu kuhusu ratiba ya mechi ya Simba dhidi ya Lipuli, ambayo ratiba ilibadilishwa kupisha ratiba ya timu ya Taifa.

  • Wachezaji wa Simba kufungiwa kucheza timu ya taifa

Msemaji wa TFF, Cliford Mario Ndimbo, ameweka wazi kuwa Mwalimu wa timu ya Taifa, Emmanuel Ammunike, hana tatizo lolote na wachezaji wa Simba, hivyo nafasi yao bado ipo timu ya taifa. Endapo wataendelea kuonyesha uwezo utakao mridhisha, wataitwa tena. Lakini pia, amesisitiza kuwa endapo wachezaji walioitwa kuchukua nafasi zao wasingekuwa wameitwa, wachezaji hao wa Simba wangeendela na programu ya mwalimu.


Tukaishangilie kwa nguvu Taifa Stars.

Sambaza....