Sambaza....

Leo kulikuwa na mkutano mkuu wa Yanga, mkutano ambao ulikuwa unafuatiliwa na watu wengi, haya ndiyo mambo matano muhimu yaliyotokea kwenye mkutano huo.

1: “Yanga imechaguliwa kuwa alama ya ukumbusho barani Afrika kama moja ya vilabu vilivyobeba alama ya uhuru wa Tanzania na uhuru wa bara la Afrika, Yanga ni klabu kubwa na yenye historia yake ndani ya nchi hii , acheni kuichukulia mzaha mzaha tu inafungwa mpaka na vitimu vidogo” waziri mwenye dhamana ya Michezo, ndugu Harrison Mwakyembe amethibitisha hilo kwenye mkutano mkuu.

2: Baraza la Wadhamini limekaa na Kamati ya utendaji na kukubaliana kurudi kwenye mfumo wa Kampuni.

3: Yanga wameunda bodi mpya ya wadhamini itakayokuwa chini ya Mzee Mkuchika, Mama Fatma Karume, Jaji Mstaafu Mkwawa, Mzee Katundu na Francis Kifukwe.

4: Yanga haijatangaza tarehe ya uchaguzi wa mwenyekiti wa klabu ambayo iko wazi kwa kipindi kirefu

5: Bodi ya wadhamini imeteua kamati maalumu kwa ajili ya kushughulikia usajili na mikataba yote ya wachezaji ambapo itakuwa chini ya mwenyekiti Abbas Tarimba, Makamu mwenyekiti Mecky sadik. Wajumbe ni:
Abdallah bin Kleib,
Nyika Hussein,
Samuel Lukumay,
Mashauri Lucas,
Yusuphed Mhandeni,
Ahmed Islam
Makaga Yanga,
Ridhiwani Kikwete,
Majid Suleiman
Ndama

Sambaza....