Ligi Kuu Bara inaelekea mwisho huku SimbaSc wakiwa katika nafasi nzuri ya kunyakua ubingwa. Achana na ligi kuelekea mwishoni, ligi nyingine ya usajili inatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Ubabe wa pesa, nguvu ya ushawishi na kukomoana vinatarajiwa kuanza tena kuelekea usajili wa wachezaji kwaajili ya msimu ujao wa ligi yaani 2018/2019!
Tovuti yako ya Kandanda inakuletea nyota kibao wa VPL wanaomaliza mikataba yao mwisho wa msimu hivyo kuweza kupatikana bure kabisa!
1. Shiza Kichuya
Alisajiliwa na SimbaSc akitokea Mtibwa Sugar kwa kandarasi ya miaka miwili. Huu ndio msimu wake wa mwisho kuitumikia klabu ya SimbaSc.
Tp Mazembe imetajwa kutaka huduma yake, pia za chini ya kapeti huenda akaelekea katika nchi ya Misri kujiunga na moja ya vigogo nchini humo.
2. Obrey Chirwa
Alijiunga na Yanga akitokea Platinum ya Zimbabwe akiunganishiwa dili na mshambuliaji mahiri ambae kwa sasa ni majeruhi Donald Ngoma.
Mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huku klabu ya SimbaSc ikitajwa kua imemalizana kila kitu na Mzambia huyo wakisubiri tuu amaliziee msimu na Yanga.
3. Ditram Nchimbi
Alijiunga na Njombe Mji akitokea Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja, huku akiwa mchezaji ghali kwenye kikosi.
Mkataba wake unakwisha mwishoni mwa msimu. Tayari msemaji wa Klabu ya SimbaSc amesikika akimsifia mchezaji huyu, huenda neema ikamwangukia mchezaji wa zamani wa Majimaji ya Songea na kusajiliwa na Simba.
4. Laudit Mavugo
Alisajiliwa na SimbaSc kwa matarajio makubwa akitoka kua mfungaji bora katika Ligi ya kwao Burundi lakini akashindwa kuonyesha cheche zake VPL.
Huenda akatemwa na Simba na nafasi yake ikachukuliwa na mchezaji mwingine wa kigeni, huku akihusishwa na kujiunga na Gor Mahia ya Kenya.
5. Kelvin Yondani
Amekua mchezaji muhimu na kiongozi Yanga kiasi cha kuiongoza timu hiyo kushiriki katika hatua ya makundi mara mbili ndani ya misimu mitatu, lakini mkataba wake unafika tamati mwisho wa msimu.
Yanga haipo tayari kumuachia haswa kutokana na kukabiliwa na hatua muhimu ya makundi shirikisho Africa na ni mlinzii pekee anaepata nafasi ya kucheza mwenye uzoefu wa michuano hiyo.
6. Mudathiri Yahya
Alijiunga na Singida utd kwa mkopo akitokea Azam fc ambako alikua hapati nafasi. Mkataba wake na Azam umeisha hivyo yupo huru kujiunga na timu yoyote.
Amehusishwa na kujiunga na Yanga na Singida utd alipo sasa. Msimu ujao huenda akacheza timu yoyote itakayokua chini ya kocha Hans Plujim (AzamFc inayosemekana amemalizana nayo au Singida utd alipo sasa).
7. Mdhamiru Yasini
Alitoka Mtibwa Sugar akajiunga na SimbaSc kwa mkataba wa miaka miwili, hivyo msimu huu ndio mwisho wa mkataba wake.
Amekua mchezaji muhimu tangu ajiunge na SimbaSc ingawa amekua hapati nafasi tangu kuwasili kwa kocha Mfaransa Pierre, lakini bado haishushi thamani yake katika klabu ya Simba.
8. Benno Kakolanya
Alikua kipa hodari wa Tanzânia Prisons kabla ya kuamua kujiunga na Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili. Amekua na maelewano hafifu na uongozi wa Yanga kiasi cha kupeleka kukitumikia kikosi hicho katika mechi chache sana.
Amekua akihisishwa na kurudi klabu yake ya zamani Tanzania Prisons pia na matajiri wa alizeti Singida utd.
9. Idd Kipagwile
Alijiunga na AzamFc akitokea Majimaji ya Songea kwa kandarasi ya mwaka mmoja ambao unaisha msimu huu. Atakumbukwa kwa goli lake dhidi ya Simba katika kombe la Mapinduzi Zanzibar.
Anahusishwa na kurudi katika klabu yake ya zamani ya SimbaSc alipopitia akiwa Simba B wakati akiwa bado kinda.
10. Kelvin Kongwe Sabato “Kiduku”
Alijiunga na Mtibwa Sugar kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kutoka kuinusuru Majimaji isishuke daraja msimu uliopita.
Mchezaji wa zamani wa Abajalo na Stand UTD amekua akifunga magoli muhimu na pia akichangia kwa kiasi kikubwa kuipeleka Mtibwa Sugar katika fainali ya Azamsports FederationCup.
Huenda akachagua kubaki Mtibwa Sugar mwakani au kusogea katika klabu kubwa zaidi ili kujitengenezea nafasi ya kuitwa timu ya Taifa.