Simba walijiandaa kushindi mechi.
Katika mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga jana 29/04/2018
katika uwanja wa Taifa Dar es salaam, umati mkubwa wa mashabiki ulikuwa ni wa Wekundu wa Msimbazi ambapo walifanikiwa kujaza uwanja kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na wapinzani wao Yanga.
Hii iliashiria Simba kujiamini kuwa wapo imara na ushindi lazima uende Msimbazi. Ushindi wa
timu ya Simba jana umemfanya abakize pointi 5 tu ili kutawazwa bingwa wa msimu huu.
Mashabiki wachache wa Yanga walijitokeza huku pia wakiwa wamekaa kinyonge na haikushangaza kuondoka mapema uwanjani.
Kukosa uzoefu katika mechi kubwa Kwa wachezaji wetu.
Siku zote mechi ya Simba na Yanga haikosagi vituko vya hapa na pale,
ingawa mechi ya jana utemi ndio ulikuwa umetawala.
Kitaalamu ni kukosa uzoefu na utovu wa nidhamu kwa wachezaji, hii inapelekea kushindwa kufanya vyema Kimataifa. Jana mapema kipindi cha pili Hassan Kessy anaonyeshwa kadi ya pili ya manjano na kutolewa kwa
kadi nyekundu kwa kucheza madhambi beki ya Simba Asante kwasi.
Pia beki mkongwe ambaye alishawahi kukipiga kunako klabu ya Simba Kelvin Yondani nae alifanya tukio la ajabu lisilo la kimpira la kumtemea mate beki wa Simba Asante Kwasi.
kwa uzoefu alio nao na kitendo alichokifanya ni chaajabu sana hii inawafunza nini vijana wanaomwangalia na kuchipukia katika tasnia yetu ya soka?
Simba ya Omog acha tu!
Katika mchezo wa jana muda mwingi timu ya Yanga imecheza pungufu. Lakini Yanga katika mchezo wa jana waliweza kutulia na kufanya mashambulizi langoni mwa Simba, inaonyesha
wazi kabisa kocha Mfaransa wa Simba hakuwa na mbinu mbadala ya kuidhoofisha kabisa Yanga na kupata ushindi mnono.
Baada ya Yanga kupata kadi nyekundu Simba ilikua inacheza pasi nyingi za kupoteza muda na kushindwa kupeleka hatari katika lango la Yanga ili kupata ushindi mnono. Hii inaonyesha wazi kua timu ya Simba inatumia mbinu za wachezaji binafsi kupigana na si ubora au sifa alizonazo kocha wao Mfaransa.
Kikosi cha Simba jana kilionyesha wazi walihitaji mtu makini wa kuchezesha katika eneo la kiungo (Ndemla au Mdhamiru). Lakini kocha huyo aliamua kubaki na wachezaji wale wale na hata alipofanya mabadiliko aliendelea kujilinda zaidi kwa kumuingiza Paul Bukaba.
Papy Tshishimbi hoi!
Kiungo huyu raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo anasifika kwa kuwa mchezaji anayekaba sana, pumzi za kutosha, stamina pamoja umahiri wake wa kupandisha mashambulizi kuanzia nyuma.
Lakini kwa jana hakika haikua siku nzuri kwake kwani alikutana na safu imara ya kiungo ya Simba chini ya Mkude na Kapombe na kumfanya Mkongo huyo kuonekana “akizurura” tuu uwanjani mpaka kupelekea kufanyiwa mabadiliko na nafasi yake kuchukuliwa na Emmanuel Martin.
Kichuya ni motoo aiseeh!!
Kiungo mshambulia wa Simba Shiza Kichuya jana aliweza kucheza kwa kiwango chá hali ya juu na kuendelea kuwanyanyasa mahasimu wao wakubwa Yanga Afrika.
Kichuya alionekana karibia kila sehemu ya uwanja na pia alifanikiwa kutoa pasi ya bao baada ya kupiga vizuri mpira wa adhabu na kumkuta Erasto Nyoni.
Anaendeleza história yake nzuri dhidi ya Yanga ya kuwatesa kila wakutanapo katika Ligi Kuu Bara. Kwani tangu ajiunge na Simba akitokea Mtibwa amekua akiwafunga au kutoa assist!.
Mchopy Shabani Nyaa