Kuelekea mtanange wa Simba na Yanga jumapili hii katika uwanja wa Taifa mashabiki wamekua na shauku yakuona ni jinsi gani vikosi vyao vitakavyopangwa siku ya mchezo.
Yanga kwa michezo ya hivi karibuni imekua ikitumia mifumo tofauti tofauti kutokana na aina mpinzani wao. Imekua ikitumia mifumo ya 4:4:2, 4:2:3:1 na 4:3:3!
Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya SimbaSc dhidi ya Yanga kikosi changu kingekua hivi.
Katika Mfumo wa 4:2:3:1:
1. Youth Rostand, 2. Juma Abdul, 3. Hajji Mwinyi, 4. Andrew Vincent “Dante”, 5. Kelvin Yondani, 6. Papy Tshishimbi, 7. Yusuph Mhilu, 8. Thabani Kamusoko, 9. Obrey Chirwa, 10. Raphael Daud, 11. Ibrahim Ajib
SUB:
R. Kabwili, H. Kessy, A. Shaibu, P. Buswita, J. Makapu, E. Martin, P. Buswita.
Jinsi mfumo utakavyofanya kazi:
Walinzi:
Mlinzii wa kulia ni Juma Abdul na kushoto ni Hajji Mwinyi ambao watakua na majukumu ya kupanda kusaidia mashambulizi lakini pia kusaidia kulinda lango lao chini ya Rostand.
Mabeki wa kati Kelvin Yondani na Andrew Vincent “Dante” hakika watakua na jukumu lá kuwadhibiti washambuliaji wa Simba John Bocco na Emmanuel Okwi. Dante ni mzuri kwa mipira ya juu ambayo ni silaha kubwa ya John Bocco huku Yondani akiwa na uzoefu wa kuwakabili na kuwadhibiti washambuliaji wasumbufu kama Okwi.
Viungo Wakabaji:
Hapa kuna Papy Tshishimbi na Thabani Kamusoko wakiwa wanacheza kama “double midfielder”. Jukumu lao kubwa likiwa kusaidia safu ya ulinzi na kuunganisha timu na safu ya ushambilliaji.
Pia viungo hawa wawili wakiwa na kazi ya kuzima mashambulizi ya Simba kuanzia eneo la katikati ya uwanja na kuwatibulia mipangoo viungo wa simba wakiongozwa na Jonas Mkude.
Viungo Washambuliaji:
Hili eneo kutakua na Yusuph Mhilu kiungo wa pembeni kulia, Ibrahim Ajibu kiungo wa upande wa kushoto na Raphael Daud Loth atakaecheza “behind the straiker”.
Jukumu kubwa la hawa watatu ni kuhakikisha beki ya Simba haipumziki kwa kupeleka mashambulizi ya kasi kila wakati.
Pia wakati timu inashambuliwa Raphael Daud na Yusuph Mhilu watashuka chini katikati na kuubana uwanja na kumuacha juu mshambuliaji mmoja akisaidiwa na Ibrahim Ajibu.
Mshambuliaji:
Obrey Chirwa atasimama kama mshambuliaji wa mwisho katika eneo la ushambuliaji la Yanga. Kasi na nguvu ndio silaha kubwa kwake hivyo viungo wa Yanga wanaweza kupiga pasi ndefu na fupi kuelekea kwa Chirwa.
Mabadiliko Ikiwa Timu Imepata Matokeo Mpaka Kipindi Cha Pili!
Mpaka kufikika kipindi cha pili katika dakika za 70 timu ikiwa inaongoza kwa mabao walau mawili sio mbaya kulinda ushindi wako.
Mabadiliko ya kwanza kabisa kufanya ni kumtoa Raphael Daud na kumuingiza Juma Makapu na kufanya kua na viungo watatu wakabaji katikati. Pia kumtoa Ibrahim Ajib na nafasi yake kuchukuliwa na Pius Buswita.
Mabadiliko Ikiwa Timu Haijapata Matokeo Mpaka Kipindi Cha Pili
Mpaka kipindi cha pili endapo timu itakua ipo nyuma kwa magoli dhidi ya Simba, njia pekee ni kujilipua na kushambulia.
Atatoka Raphael Daud na kuingia Emmanuel Martin huku Ajibu akiingia ndani kucheza pacha na Chirwa na Emmanuel kwenda kucheza pembeni. Pia kuongeza kasi pembeni ataingia Pius Buswita kuchukua nafasi ya Yusuph Mhilu.