Sambaza....

Liverpool alicheza mfumo wa 4-3-3 na Manchester United katika karatasi alionekana kucheza mfumo wa 4-3-3 lakini uwanjani ilikuwa tofauti, wakati wanashambuliwa walikuwa wanacheza mfumo wa 4-2-3-1.

Ila wakati wa kujilinda Manchester United walikuwa wanacheza mfumo wa 4-5-1.

Kipi kiliwasaidia Manchester United wakati wanajilinda ?

Moja ya makosa ambayo timu nyingi hufanya kipindi ambacho zinakutana na Liverpool ni kutengeneza uwazi eneo la nyuma.

Na hii inatokana na wachezaji wa mbele wa Liverpool kutopenda kusimama eneo moja , hivo kuwalizimu mabeki kuwafuata na wanapokuwa wanawafuata kuwakaba ( ku mark man to man) hujikuta eneo lao la nyuma wametengeneza uwazi.

Hiki kitu leo hii Machester United hawakuruhusu. Mabeki wao hawakutengeneza uwazi eneo la nyuma hivo kuziba mianya, na hakukuwepo mianya ambayo ingewawezesha washambuliaji wa Liverpool kupenya.

Hata mabeki wao wa pembeni ( Ashley Young na Antony Valencia) hawakuwa wanawapanda juu kusaidia mashambulizi, kutopanda kwao mbele kulisababisha timu yao kutotengeneza uwazi au mianya eneo la nyuma, hivo ilikuwa ngumu kwa kina Mohamed Salah, Saido Mane na Roberto Firmino kupata mianya ambayo ingawawezesha wao kupenyeza.

Na hawakupewa uhuru mkubwa sana kwa sababu waliwakaba “man to man” tena kwa utulivu, na hii ikawanyima uhuru kina Mohamed Salah

Lipi lilikuwa kosa la Liverpool kwa upande wa ulinzi ?

Wakati Manchester United wakiwa imara katika eneo la ulinzi na kuhakikisha hawatengenezi uwazi au mianya eneo lao, lakini ilikuwa tofauti kwa upande wa Liverpool.

Mabeki wa Liverpool walikuwa wanatengeneza uwazi ambao uliwafanya washambuliaji wa Manchester United kuwa huru, mfano goli la kwanza la Manchester United, wakati De Gea anapiga mpira kwa Lukaku, Lovren aliondoka eneo lake la nyuma na kumfuata Lukaku aliyekuwa amesogea mbele kidogo, baada ya Lovren kuondoka aliacha uwazi eneo la nyuma, uwazi ambao aliutumia Rashford ambaye wakati anapokea mpira alikuwa peke yake akiwa huru. Goli la pili pia, wakati Rashford akipokea mpira alikuwa eneo wazi ambalo lilimfanya awe huru.

Kipi kiliwasaidia Manchester United wakati wanashambulia?

Jose Mourinho alipanga kutumia mashambulizi ya kushtukiza leo, alihakikisha hatumii mabeki wake wa pembeni kushambulia ila alitaka kutumia viungo wake kama waanzilishi wa mashambulizi huku akihakikisha pembeni kushoto ameweka mtu mwenye mbio (Rashford) ambapo hata Alexis Sanchez alikuwa anaenda upande huo kuongeza nguvu, hivo ikawa mzigo kwa Alexander Anold.

Kipi kiliwagharimu Liverpool wakati wanashambulia?

Walitegemea kupitishia mashambulizi katikati ambapo Manchester United walikuwa wengi kwani wakati wanakaba walikuwa watu tisa nyuma ya mpira katika mfumo wa 4-5-1. Njia pekee ilikuwa wao kulazimisha kupitia pembeni.

Ambapo kipindi cha pili walifanya hivo, ambapo walianza kutia presha eneo la Liverpool kupitia pembeni mpaka Liverpool wakajifunga.

Ingizo la Lallana lilikuwa na dalili ya kuonesha kuongeza nguvu kwa Liverpool, lakini Jose Mourinho aliamua kumtoa Rashford na kumwingiza Fellain ambaye aliongeza idadi ya watu katikati na hali ambayo ilikuwa ngumu kwa Lallana kuisaidia timu kwa kiwango kikubwa.

Sambaza....