Sambaza....

Jose Mourinho anaweza kumaliza uteja kwa Jurgen Klopp?

Alama mbili pekee zinawatenganisha hawa watu na wako kwenye vita ya kupigania nafasi ya pili mpaka sasa.

Wanakutana katika uwanja wa Old Trafford, mechi ya kwanza walitoka suluhu. Jose Mourinho anamkaribisha tena Jurgen Klopp katika uwanja wake wa nyumbani, kipi kitakuwa nguvu kwake leo?

Mechi nyingi msimu huu mtu pekee ambaye amekuwa akiwapa uhai Machester United na kuiweka timu mchezoni kwa muda mrefu ni golikipa David De Gea

Amekuwa mlinzi dhabiti wa kikosi cha Manchester United, ulinzi wake umeifanya timu kuwa salama na kuwa ndani ya mchezo kwa muda mrefu.

Maendeleo ya Safu mbili za Ulinzi yakoje kwa timu zote mbili??

Tangu Liverpool wamnunue Van Djik wamenufaika kwa kiasi kikubwa sana, timu imekuwa haina makosa mengi binafsi nyuma, hata aina ya magoli waliyokuwa wanafungwa awali kwa sasa yamekuwa nadra sana.

Mfano kabla ya Van Djik , Liverpool walikuwa wakiruhusu magoli yanayotokana na Krosi au kona. Lakini tangu aje imekuwa nadra kuona Liverpool wakiruhusu aina hiyo ya magoli kwa sababu Van Djik amekuwa madhubuti kuokoa mipira hiyo.

Liverpool katika michezo 6 iliyopita amefungwa magoli matatu tu na kuondoka na clean sheets nne.

Wakati Manchester United imeruhusu magoli manne na kuondoka na Clean sheets tatu katika michezo hiyo sita iliyopita.

Kwa hiyo kwa hivi karibuni safu ya ulinzi ya Liverpool imekuwa imara na isiyokuwa na makosa mengi binafsi ukilinganisha na safu ya ulinzi ya Manchester United.

Manchester United kuingia kama “underdogs” itakuwa na msaada kwao ?

Bila shaka Manchester United leo hii ni “underdogs” kwenye mechi ya leo, hii inaweza ikawa na faida na hasara

Faida inakuja pale Manchester United watakapokubali kupokea hali hiyo, hii itawasaidia kuwaheshimu Liverpool. Kitendo ambacho kitajenga nidhamu na umakini ndani yao

Presha kubwa haitokuwa ndani yao, hali ambayo itawafanya wawe na utulivu kwa ƙkila nafasi wanayoipata

Hasara ni pale watakapokuwa ogopa hiki kitawafanya wawe na maamuzi yaliyo na upungufu wa umakini ndani yao.

Hivo wanatakiwa wakubali hali ya wao kuwa underdogs katika mechi hii.

Ukitoa De Gea Upi uimara wa Manchester United?

Kuwa na wachezaji tofauti wa kubadili matokeo. Mfano katika mechi mbili zilizopita kumekuwa na aina tofauti ya watu waliohusika kubadili matokeo ya Manchester United

Mechi ya Chelsea Lukaku na Lingard walikuwa chachu ya ushindi wa Manchester United kwa kutoka nyuma ya goli moja

Mechi ya Palace walitoka nyuma ya magoli mawili na wakashinda, mtu aliyebadili matokeo ni Nemanja Matic.

Hii inatosha kukuonesha kuwa Manchester United ina watu wengi wanaoweza kubadili matokeo ndani ya dakika tisini.

Upi ubora wa Liverpool?? Hapana shaka safu yao ya ushambuliaji ni safu bora kwa sasa , kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu huu katika mechi nane walizocheza wamefanikiwa kufunga magoli 28 ikiwa ni timu iliyofunga magoli mengi zaidi, kwenye ligi kuu ya England ndiyo klabu ya pili kwa kufunga magoli mengi nyuma ya Manchester City.

Aina yao ya kushambulia kwa kasi ndiyo ubora wao unapoanzia.

Kipi wakifanye Manchester United ?

Cha kwanza ni kuweka ulinzi dhabiti ili kutetengeneza uwazi katika eneo lao la nyuma , uwazi ambao utatumiwa na wachezaji wa Liverpool kuwaadhibu.

Roberto Firmino amekuwa chachu kubwa kule mbele kulingana na aina ya mchezo anaocheza, anacheza kama false 9 hali ambayo inamfanya ashuke chini, kila akishuka chini katikati lazima beki wa timu pinzani ashuke kumkaba, akishuka naye kule nyuma huacha uwazi, uwazi ambao unatumiwa na kina Saido Mane na Mohamed Salah, hivo Manchester United wanatakiwa kuepuka kutengeneza uwazi eneo lao la nyuma.

Pia kwa sababu Liverpool hushambulia kwa kasi hali ambayo hufanya kutojidhatiti nyuma. Hivo Manchester United wakicheza mashambulizi ya kushtukiza inaweza ikawa na faida kubwa kwao.

Kipi wakifanye Liverpool?

Juu nimemwelezea Roberto Firmino, huyu ndiye mchezaji muhimu kule mbele asiyeangaliwa sana. Kumtumia kama false 9 kutakuwa na faida kubwa kwao kama nilivyoelezea huko juu.

Sambaza....