Sambaza....

Hutokea mara chache sana kwa kijana chipukizi aliyeaminika na kutekeleza kile ambacho kocha alikitarajia, na vile vile hutokea mara chache sana kwa kocha kuendeleza kiwango cha chipukizi mwenye kipaji halisi cha soka .

Akiwa na umri wa miaka 18 kwenye kombe la Dunia mwaka 1998 nchini Ufaransa, kocha wa timu ya taifa ya uingereza Glenn Hoddle alimuamini kijana aliyetoka kufanya makubwa na klabu yake ya Liverpool, msimu wa 1997 mbele ya majemedali wawili Alan Shearer and Teddy Sheringham

Alimuamini na alimpa nafasi na kisha Michael Owen hakumungusha na atakumbukwa kwa bao tamu zaidi alilofunga dhdi ya Argentina huu ndio mwanzo wa Michael kuanza kutengenza Jina duniani

Ni kama Lionel Messi na Pep Guardiola … ni rahisi tu .. alimjengea imani na kisha Messi hakumungusha .. kuna mtu mmoja aliwahi kusema “Golden fish has no hiding place” akimaanisha “Samaki mzuri au kitu kizuri huwa hakijifichi” Ni kama kipaji huwa akijifichi kikubwa ni kukiendeleza

Sidhani kama kuna mtu anamashaka na Kipaji halisi cha Marcus Rashford anakipaji halisi, anakasi nzuri, uwezo wa kupiga chenga, kumiliki mpira na vile vile anauwezo wa kucheza nafasi zote za mbele sehemu ya ushambuliaji. Kipaji halisi alichokiibua Lous Van gaal

Rashford alifanya makubwa sana chini ya van gal na alionyesha kuwa na utulivu wa hali ya juu akiwa kinda mwenye umri wa 18 na siku 12 tu, dunia nzima tulikua tumeshakiona kipaji chake

Marcus Rushford akishangilia moja ya magoli yake

Wengi watamkubuka kwa mabao mawili aliyoyafunga dhidi ya Arsenal Februali 28, 2016 na bao pekee alilofunga kwenye mchezo wa Manchester derby Machi 20, 2016 na kuifanya klabu ya Man United kupata ushindi wake wa kwanza kwenye uwanja wa ugenini dhidi ya Manchester City toka mwaka 2012, pia mchezo huo ulimfanya aweke rekodi ya kuwa kijana mdogo zaidi kufunga bao kwenye mchezo wa Manchester Derby, akiwa na umri wa miaka 18 na siku 141

Nini ambacho Van gal alifanya kwa Marcus Rashford, kwanza alimjenga kisaikoloji, pili akamuamini na akampa nafasi na kisha Rashford hakumuangusha kwa kuonyesha kile ambacho alichonacho

Huu ni msimu wa pili Marcus Rashford akiwa na Jose Mourinho kumbuka baada ya Luis van gal kuondoka na Jose Mourinho kutangazwa kuwa ndiye mlithi nafasi ile, watu wengi hasa wachambuzi wa soka na wakongwe wa klabu ya Manchester United waliamini kuwa huu ndio mwisho wa Rashford kutokana na historia ya Jose Mourinho kutokua na imani na wachezaji makinda, na kuwa na tabia ya kuijenga timu kwa kununua wachezaji waliokamilika

Swali la kwanza ambalo Jose Mourinho aliloulizwa na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa kuwa kocha mkuu wa mashetani hao wekundu …Ni namna gani atandeleza vipaji vya wachezaji chipukizi walioibuliwa kutoka kwenye academi ya Manchester United ambao van gal aliowaacha hasa wakimanisha Rashford, Jose aliwajibu kuwa ataendeleza pale ambapo Van gaal alipoishia

Msimu wa mwaka jana mchezaji ambaye aliyeonekana kuibeba zaidi ManchesterUnited nyuma ya Zlatan Ibrahimovich ni Marcus Rashford

Alionyesha okumavu wa hali ya juu alifunga mabao muhimu kwenye michezo muhimu, yani kwa ufupi aliendeleza kiwango maradufu zaidi ya kile ambacho aliokionesha akiwa chini ya Van Gaal

RASHFORD ni mchezaji ambaye aliefuta nyao za makinda wenzake walioanza vizuri kwa kukuza kiwango kwa njia ya uratibu, yani kila mwaka alionesha utofauti wa kiuchezaji . Kiwango alichokionesha msimu akiwa na Van Gal ni fofauti na kile alichokionyesha chini ya Jose Mourinho kila msimu alikua anapanda, watu wengi waliamini msimu huu wa tatu ndio atakua moto zaidi na kuelekea kwenye ubora .

Lakini picha na ndoto zake ni kama zimeyeyuka, tulichokitegema kimekuja tofauti, msimu wa mategemeo ndio umekua wamachungu kwake

Kila nikiangalia nafasi ya Rashford kwenye kikosi cha Mancherster United chini ya Mourinho siioni ..
kwanini nasema hivyo..Rashford hayupo sawa,uso wake hauna tena furaha,anacheza akiwa na mawazo mengi sana

Marcus Rashford anatatizo moja kubwa tatizo la saikolojia, Rashford ni yule yule wa Van Gal na wa msimu jana na wala hajashuka kiwango, ila tatizo hayupo sawa kichwani .. na ndio maana akipewa nafasi unamuona anataka kufanya kitu cha ziada ambacho hakiwezi, analazimsiha kufunga kwenye mazingira magumu yaani amekua hafikiri kabla ya maamuzi,anapiga mipira hovyo na mwisho wa siku anapokonywa mipira kijinga

Rashford anahitaji matibabu ya saikolojia tu, na mtu ambaye atakaye mtibu kwa ukaribu ni Jose Mourinho lakini Jose Mourinho huyu, ni kama hana muda na Rashford yani hana imani kubwa katika Rashford na ndio maana anahitaji wachezaji zaidi katika nafasi yake

Yule Mctominay sio kusema anakipaji halisi kikubwa sana hapana anakipaji lakini cha kawaida

Alichokifanya Mourinho ni kumjenga kisaikolojia tu kuwa anaweza na amemuhakikishia namba endapo hato muangusha, Mourinho haishi kumuongelea Mctominay kwa kumsifia kila anapongea na waandishi wa habari

Mourinho amemtenegeza Mctominay kuwa anajua kuliko Pogba au Hererra

Jiulize kama Mourinho ameweza kumtengenza kisaikolojia Mctominay kwanini asiweze kwa Marcus Rashford ambaye anaonekana hayupo sawa

Jibu ni rahisi tu …. haamini katika Rashford….. Rashford anatakiwa afuate nyayo za akina Mohammed Salah… anatakiwa aondoke tu Manchester United msimu ujao kama kweli anahitaji kuwa bora zaidi ya hapo alipofikia, sema anatakiwa achague sehemu sahihi atakapo pata nafasi ya kucheza akiwa huru muda mwingi

Chini ya Jose Mourinho sioni Rashford kurudi kwenye hali yake ya misimu miwili iliyoisha simaanishi Mourinho ni kocha mbaya, ila hawa makocha huwa wana watu wao wanaowapenda na ndio maana Conte ametuaminsha David Luiz si chochote kwa Andreas Christensen.

Akiwa na miaka 20 tu Rashford anahitaji kocha atakaye muamini na kumpa nafasi zaidi kama Pep alivyofanya kwa Lionel Messi, kama Antonio Conte anavyomuamini Andreas Christensen …

kijana ukimuamini hatokuagusha…

Marcus Rashford jitafakari upya kisha angalia nini unataka zaidi ya hapo ulipo

Sambaza....