Sambaza....

Licha ya kuwa na CV nzuri na uzoefu katika soka nini kilikuwa kikwazo katika timu ya Simba hususani katika mechi yao dhidi ya Almasry ya Misri?

Kwa mawazo na mtazamo wangu ilikuwa game ya wazi na ya ushindi kwa Simba ikiwa ipo nyumbani na kikosi cha wachezaji 12 (na mashabiki). Na baada kugundua hilo waarabu walikuwa na plan B yaani mbinu mbadala kutaka kumvuruga mwamuzi wa mchezo kutoka Afrika Kusini Thando Helpus Ndzandzeka na kupoteza muda muda ili kuipooza Simbasc.

Image result for simba vs almasry images

Lakini licha ya yote hayo Simba walikuwa hawana cha kupoteza baada ya kutokushiriki mashindano makubwa kwa kipindi kirefu. Sikuona sababu ya kocha wa Simba raia wa Ufaransa Pierre Lechantre kucheza na mabeki watatu yaani Kotei, Mlipili na Nyoni huku nafasi ya kiungo ikichezwa na Kapombe na Mkude kwanini?

Mchezo wa kimataifa kama ule Simba ilipaswa kutuonyesha ubora na thamani ya kikosi walichonacho kwani kuna wachezaji mahiri ambao wangewafanya wana Simba kibuka kidedea.

Aina ya mfumo ambao Simba walitumia jana 3-4-3 lakini kwanini haukuwa 4-2-1-3, ni sawa kutumia mfumo walioutumia lakini kadri mchezo ulivyokuwa ukiendelea huu mfumo wa 3-4-3 hakuwa mfumo sahihi kwani hakukuwa na ule muunganisho sahihi baina ya viungo wa Simba na washambuliaji wake hii ilitokana na kumchezesha kapombe katika nafasi ya kiungo ikimtegemea yeye kupandisha mashambulizi.

‘’Perfect’’ Mkude katika timu ya Simba mchezaji pekee mwenye kuonyesha uwezo wa hali ya juu japo wengi wanaweza wasilitambue hili kutokana na kufanya yanayohitajika kufanya na wachezaji makini kama yeye ananikumbusha mtu kama Michael Carrick wa Manchester united, mchezaji ambaye anaweza kutuliza presha ya mchezo, kujua huu mchezo unataka nini na kwa wakati gani. Perfect Mkude lakini angempata mtu kama Ndemla au Mzamiru mbele yake tungekuwa tunasimulia mengine sasa.

Tactically Simba walizidiwa hivyo kocha Pierre Lechantre alipaswa kuliona hili mapema na ndio maana Simba walikuwa wanapiga pasi nyingi lakini kwenye eneo lao na si kusogea mbele, mimi nadhani laiti kama wangeweza kucheza mfumo wa 4-2-1-3 ambapo Kapombe, Nyoni, Mlipili, na Kwasi wakitengeneza nafasi ya ulinzi, holding Mkude na Kotei mbele yao Ndemla washambuliaji Okwi, Kichuya na Bocco mwarabu asingeambulia chochote.

Image result for simba vs almasry images

Sasa tujipange na mchezo wa marudiano hiyo March 17 Cairo Misri. Je Simba ataweza kufanya maajabu?. Ataweza kurudia yale ya Zamalek na Ismailia?.
Let’s wait and see.

Mchopy Shabani Nyaa.

Sambaza....