Mchezo wa soka ni taaluma kamili inayojitegemea ambayo ina misingi yake mikubwa kwenye soka la vijana, ambayo wachezaji wadogo au vijana huanza hatua yao ya kwanza kwenye soka, lazima tukubali kuwa hakuna njia ya mkato kwenye mchezo soka, nchi yoyote inayotaka mafaniko yake lazima ipite katika misingi sahihi
Katika kipindi hichi hutokeaga hatua za awali kabisa za michezo ya watoto wa kiume au wa kike kwa kupata mafunzo ya kiufundi, kimbinu, kitambuzi na kisaikolojia huanzia chini na hili lazima lifanyike nchi nzima kwa kuwa na mtahala mmoja wa kufundishia unaofaa kulingana na aina ya watoto tuliyonao kiulewa, kiakili na vile vile maumbo yao, lakini pia ikiwa ni pamoja na kuchagua aina gani ya uchezaji ambao utaendana na wachezaji tulionano (Tactical philosophy)
hapo tunaanza kuwatengeneza kushiriki katika shughuli za kuja kuwa wachezaji wakubwa mwenye muongozo mzuri wa hali ya juu kabisa wenye kiwango na mahitaji thabiti kwenye mchezo wa soka
Katika makala hii nataka kutahadharisha mashabiki na viongozi na wahusika wengine kwenye soka, wajue umuhimu wa kazi nzuri ya maendeleo ya timu za vijana kwa hapo baadae ni kupata matunda mazuri ya wachezaji wazuri nchini, na kinyume chake kwa maana ya kupuudhia hili ni kufeli katika mpangilio mzima wa mchezo wa soka nchi nzima.
Vijana wakiandaliwa vema ni uti wa mgongo wa soka kwa hapo baadae vilabu vya soka na timu za taifa kwa jumla, hupata wachezaji wazuri waliondaliwa kitaalam katika nyanja zote
Umuhimu wa timu za vijana unatakiwa kuwepo katika kipindi chote cha mchakato wa wao, kujiendeleza ambayo itapelekea wachezaji vijana kuonyesha mazingira yao ya kujitolea, na uchunguzi wa uwezo wao na wakati huo huo kuwa na ushindani wa hali ya juu,
kazi ya kutengeneza mchezaji mwenye kuja kuleta mavuno ya juu huanza mapema kwa kuanzia mashuleni, vituo vya michezo ya soka, na hata kwenye vilabu vyenye timu za vijana
Kipindi cha vijana kujifunza ni muhimu sana wafundishwe mambo yote ya msingi ya mchezo wa soka, ili hapo baadae akiwa mchezaji mkubwa hatokuwa na mapungufu ambayo kwa wakati mwengine kwa yule kijana ambaye kaibuka kwa kipaji chake cha asili na hakupitia mafunzo yoyote ya awali kocha wake hulazimika kumfanyia mazoezi binafsi, ili kusawadhisha mapungufu aliyoyaona ila akiwa aliandaliwa mapema kitaalam na kupata mafunzo yote ya msingi yaliyofanyika wakati mwafaka katika mchakato wa maendeleo ya kijana akiwa na kipaji binafsi cha asili basi kazi uwa nyepesi kwa kocha kwani mchezaji anakua amekamilika
Katika hatua hii hutokea bila kuwa na wasi wasi ya matukio makubwa ambayo kwa uhakika hutokea hapo baadae, kwa vile vijana wameandaliwa katika mazingira mazuri ya kitaalam kila mara upungufu wa ufatiliaji wa maendeleo morphological lazima yawe ya ujasiri kwa upande wa makocha, makocha wa viungo, wanasaikolojia nk.. Kwani kipindi hichi na siku zijazo inaweza kuleta matokeo mabaya kwenye mafunzo ya mchezaji.
Ngazi ya timu za vijana yana ulazima wa kujua ni aina gani ya wachezaji tulionao na tunaotaka kupeleka katika soko la mchezo wa soka, kwa kuwa na chombo cha kupanda kikundi kitakachotoa wataalamu moja ya mikutano itakua ya kuanza kutoa tathmini ya kikosi cha wachezaji wa sasa wenye hari ya kitaalam zaidi, kwa maana hiyo ni muhimu majukumu za vijana ni kutengeneza wachezaji bora wa baadae ambao Kama tulivyosema walikua na vipaji vyao vya kuzaliwa baada ya kuandaliwa vyema kitaalam wanakuwa wachezaji waliokamilika na mwenye mawazo ya ushindi mda wote
Hutuwezi kuwa ligi bora Kama hatuna timu bora na hatuwezi kuwa na timu bora, kama hatuna wachezaji bora na hutuwezi kuwa na wechezaji bora kama hatuna timu za vijana bora tuzingatie hili kwa umuhimu wa kipekee ndio uti wa mgongo wa mchezo wa soka popote pale ulimwenguni, kwa maana hiyo tukiwa na ligi bora na timu bora na wachezaji bora bila shaka tutakua na timu za taifa bora za vijana na wakubwa.