Shirikisho la Kimataifa la Historia ya mpira wa miguu na takwimu Duniani (IFFHS) limeitangaza chati ya vilabu bora duniani kwa mwaka ambapo kwa Tanzania Yanga imeibuka kinara ikiwa katika nafasi nzuri zaidi akimzidi mtani wake Simba.
Simba na Yanga ikiwa ndio miamba ya soka nchini huku kwa miaka ya karibuni wakifanya vyema kitaifa na kimataifa kwasasa. Katika takiwmu hizo za IFFHS zimeonyesha Yanga kuwa ni Klabu namba tatu kwa ubora Afrika na Simba SC namba 12.
Takwimu hizi ni kwa kipindi cha kati ya September 01, 2022 hadi Augst 31, 2023, huku vilabu vya Kaskazini vikiojekana kutawala katika nafasi za juu kwenye takwimu hizo zilizotoka hivi karibuni.
Katika chati hiyo namba moja ni Al Ahly ya Misri na Wydad Casablanca ya Morocco huku namba kumi ikishikwa na USM ya Algeria ikikamilisha kumi bora ya vilabu kwa Afrika.
List kamili ya vilabu 12 bora hii hapa:
- 1. Al Ahly
- 2. Wydad Casablanca
- 3. Yanga Sc
- 4. Pyramids
- 5. Mamelodi Sundowns
- 6. FAR Rabat
- 7. Raja Casablanca
- 8. Zamalek
- 9. CD Belouzdaid
- 10. USM Algier
- 11. Esperence de Tunis
- 12. Simba Sc