Sambaza....

Mtanange wa soka kati ya Simba sc dhidi ya Azam fc umemalizika kwenye uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam kwa Simba sc kuibuka wababe kwa ushindi wa bao 1-0

Alikuwa ni Emmanuel Okwi aliweza kuwapa furaha mashabiki wa Simba hii leo, baada kuitumia vema pasi ya Asante Kwasi.

TATHIMINI

Nikianza na wenyeji Simba sc ambao waliingia uwanjani wakitumia mfumo wa 3-5-2, ukuta wa nyuma ukiwa na walinzi watatu Erasto Nyoni, Yusuf Mlipili na James Kotei

Eneo la kiungo Jonas Mkude(kwangu Mimi ndiye mchezaji bora wa mechi) alicheza kama kiungo wa ulinzi ambaye pia alikuwa na majukumu ya kucheza kama box to box midfield huyu ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuipoteza Azam katikati ya kiwanja, alisimama kama kiungo wa ulinzi pale inapopoteza mpira pia alijenga mashambulizi ya kati kama kiungo mchezeshaji akitoa back up kwa Said Ndemla huku Shiza kichuya akicheza kama kiungo mchezeshaji wa pembeni kulia akiingia ndani ili kuongeza namba kwenye eneo la mwisho.

Asante Kwasi na Shomari Kapombe hawa walisimama vema kwenye ile wing back style na kuhakikisha timu inashambulia mpaka mwisho.

Mbele walisimama John Bocco kama mshambuliaji wa mwisho na Emmanuel Okwi alicheza kama deep playmaker huyu alitumika kama daraja la viungo wa kati na safu ya ushambuliaji huku akifanya switching na Bocco kama mshambuliaji wa mwisho.

Hakika Simba walikuwa bora sana kimbinu na kiufundi huku silaha ya kwanza ilikuwa ni kuhakikisha wanamiliki mpira kitu ambacho walifanikiwa hasa kipindi cha kwanza, waliweza kutoka counter attacking play ama kwa short pass style mara kwa mara walikifumua kiungo cha Azam na muunganiko huu wa kimbinu uliweza kuwasaidia kupata bao baada ya Erasto Nyoni kupiga Penetration pass kwenda kwa Asante Kwasi aliyepiga V pass ambapo Okwi akiwa kwenye attacking run nzuri aliweza kufunga.

Kwa hakika Simba walistahili ushindi katika mchezo wa leo authority yao ya mchezo ilikuwa nzuri sana, tactical philosophy, tactical focus, changing position na style of play ni vitu vilivyoiwezesha kupata ushindi hii leo.

Azam fc wao waliingia kwenye mchezo huo kwa kutumia mfumo wa 4-2-3-1 (unconventional formation) nyuma kukiwa na walinzi wanne Bruce Kangwa na Daniel Amoah kama walinzi wa pembeni huku Agrey Morris na Yakub Mohammed wakicheza kama walinzi wa kati hile ni eneo ambalo madhaifu yake yamechangia Azam kupoteza mchezo.

Kushindwa kufanya pre marking, kwa hakika hawakuwa vizuri kumkaba mtu asiye na mpira achilia mbali goli alilofunga Okwi lakini mara kwa mara walirudia makosa haya na nusura Okwi awaadhibu tena kwa free header.

Kwenye eneo la kiungo kwa kiasi fulani walijitahidi kukaba lakini mara nyingi walizidiwa na idadi kubwa ya viungo wa Simba na aina ya uchezaji wao.

Stephen Kingue na Frank Domayo kwa pamoja walicheza vizuri kama double pivot lakini tatizo kubwa walikosa msaada kutuko kwa watu watatu wa juu, Iddi kipagwile, Yahya Zayed na Enock Atta hawakuwa na ubora pale timu ilipopoteza mpira.

Kukosa ubunifu kwenye eneo la ushambialiji ni tatizo ambalo lilifanya safu nzima ya ushambuliaji kupotea, hasa pale walipojaribu kwenda kwenye attacking adminstration kwa high balls aina hii ya mipira ilionekana kukosa faida kutokana na aina ya mshambuliaji wao wa mwisho.

Azam walikosa ubora kwenye man to man defensive system, attacking tactics, pressing game na kasi yao haikuwa nzuri sana kuanzia mwanzo mpaka mwisho mara nyingi walipooza pale walipofika kwenye eneo la 18, ya Simba.

Sambaza....