Kocha Nabi alijiunga Yanga tarehe 19/04/2021 akichukua nafasi ya Cedric Kaze (Kazelona) aliekua kocha mkuu wa Yanga kwa kipindi kile na kutimuliwa halafu akarudishwa baadae kama kocha msaidizi wa Nabi.
Tarehe 20/04/2021 Yanga walikua na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Gwambina fc pale kwa Mkapa na Yanga walishinda 3-1, Nabi alikua jukwaani.
Mchezo wa kwanza kwa Kocha Nabi ulikua dhidi ya Azam Fc Ligi kuu Tanzania Bara na Matokeo Yanga ilipasukua 0-1 goli la Dube, baada ya hapo Yanga haikupoteza tena mchezo wa ligi kuu hadi baada ya mechi 49 (Unbeaten) waliyokuja kuivunja Ihefu fc kwa ushindi wa 2-1.msimu huu wa 2022/23.
Takwimu za Nabi akiwa Yanga.
Ligi kuu
Msimu 2020/2021
Mechi 6 Ligi kuu!
Ushindi 4 ( 1-0 dhidi ya Mnyama) sare 1, kipigo 01, magoli ya kufunga 09 na karuhusu goli 05
Mechi 3 ASFC alishinda dhidi ya Mwadui, Biashara na Prisons na kupoteza fainali dhidi ya Mnyama Simba 1-0 Kigoma.
Msimu 2021/2022
Mechi 30, ushindi mara 22, sare 08 na kupoteza 0, magoli ya kufunga 49, karuhusu 08, alama 74.
Msimu wa 2022/23
Mechi 30, ushindi mara 25, sare 3, kupoteza mara 2, magoli ya kufunga 61 na karuhusu magoli 18, alama 78.
Kimataifa
Ligi ya mabingwa mechi 6 hatua ya mtoano.
Ushindi mara mbili dhidi ya Zalan Fc
Vipigo vitatu dhidi ya Rivers United (nyumbani na ugenini) na Al-Hilal mara moja na sare moja dhidi ya Al Hilal. Magoli ya kufunga 10 na yakufungwa manne.
Shirikisho Afrika: Kuanzia mtoano hadi Fainali
Mechi 14, kushinda mara 09, sare 03, kupoteza mara 02 ( US Monastir na USM Algier). Magoli ya kufunga 17 n yakufungwa magoli 07.
Michuano ya Kombe FA.
Mechi 14, ushindi mechi 13, kupoteza mara moja (Fainali dhidi ya Simba sc 1-0.)
Mafanikio.
Ubingwa ligi kuu Bara mara mbili.
Ubingwa ASFC mara mbili.
Medali ya CCF mshindi wa pili.
Kocha bora wa msimu mara mbili
Ngao ya Jamii mara mbili.
Utamkumbuka kwa tukio lipi alilokukosha sana akiwa Yanga Profesa Nabi!?
Credit to: Anuary Binde (Mzee wa takwimu)