Sambaza....

Klabu ya JKT Queens imefanikiwa kuibuka na ubingwa wa Ligi kuu ya Wanawake baada ya kufanikiwa kupata ushindi katika mchezo wake wa mwisho waliokua ugenini dhidi ya Mkwawa Queens ya Iringa.

Kwa ushindi huo JKT Queens wamemaliza na alama 46 alama moja zaidi ya Simba na kuwafanya kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Wanawake na kuvunja utawala uliowekwa na Simba Queens miaka ya hivi karibuni.

Simba Queens walikua wametwaa ubingwa huo mara tatu mfululizo na mara moja walifanikiwa kuiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa wanawake na walifika hatua ya nusu fainali.

Nahodha wa JKT Queens Deonisia Minja akikabidhiwa kombe la ubingwa na mgeni rasmi.

JKT Queens ambao wamechukua ubingwa bila kupoteza mchezo hata mmoja sasa watahamishia nguvu zao katika michuano ya kanda ya Cecafa ili kupata mwakilishi ambae atakwenda kuiwakilisha kanda hii katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aidha katika Ligi pia mshambuliaji wa Simba Jentrix Shikangwa ameibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao 17 na kuwaacha Deonisia Minja mwenye mabao 16 na Stumai Abdalla mwenye mabao 13 wote kutoka JKT Queens pamoja na Winfrida Charles kutoka Allaince akiwa na mabao 13. 

 

Sambaza....