Sambaza....

Klabu ya Yanga imeshaanza kimyakimya usajili kuelekea msimu ujao ambapo tayari jicho lao limetua kwa nyota wa zamani wa Timu ya Taifa ya Zimbabwe na winga wa Kazier Chiefs Khama Billiant ambae mkataba wake unaelekea ukingoni.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Zimbabwe kusalia kwa Chiefs imekuwa ngumu na haitashangaza ikiwa klabu haitaongeza mkataba wake msimu huu, majeraha yamezidisha hatima yake kuwa ngumu kwani amekosa mzunguko mzima wa pili wa msimu huu.

Kazier Chiefs hivi majuzi walisema Billiat ameanza mazoezi, lakini bado haijafahamika kama atakuwepo kwa mechi yao ya mwisho ya msimu huu. Mabingwa wapya wa Tanzania, Young Africans wamethibitisha kumtaka nyota huyo wa zamani wa Ajax Cape Town.

Khama Billiant

Rais wa klabu hiyo Mhandisi Hersi Ally Said aliiambia FARPPost kwamba Billiat alikuwa kwenye rada zao. Hata hivyo, alisema walikuwa wakifuatilia hali hiyo ili kuona ikiwa Chiefs itaongeza mkataba wake. “Ukiniuliza (kuhusu Billiant), yeye ni mmoja wa wachezaji ninaowapenda. Aina ya ubora alionao ni wa nje ya dunia hii. Kwa hivyo, kwa nini hapana, ikiwa tunaweza kupata nafasi yakumsajili?.”

Yanga ipo katika kuendelea kukisuka kikosi chake wakitaka kusajilo wachezaji wenye uzoefu zaidi ili kufanya vyema katika Ligi ya Mabingwa Afrika tofauti na ambavyo walitolewa mapema katika msimu huu.

Wananchi wamepanga kuachana na winga Benard Morrison hivyo mapema wameanza kusaka mbadala wake na moja ya mawinga hatari Afrika ni pamoja na Khama Billiant raia wa Zimbabwe anaetajwa na Wananchi kwasasa.

Sambaza....