Sambaza....

Hatimae fainali za msimu wa mwingine wa sodo beach soccer zimemalizika siku ya Jumamosi na Timu ya Waandishi wa habari za michezo wakiibuka kinara na kubeba ubingwa huo kwa timu zote mbili.

Haikua safari rahisi kwa Timu hiyo ya Waandishi wa Habari za michezo kupata ubingwa huo tena kwa timu zote mbili kwa upande wa wanawake na wanaume na kujizolea zawadi ya pesa taslimu.

 

Kwa upande wa timu ya wanaume ya Waandishi wa habari za michezo haikua rahisi kuweza kunyakua ubingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na kuratibiwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Betika.

TImu hiyo ilinza kuwatoa IPP Media katika mchezo wa robo fainali baada ya ushindi wa mabao manane kwa bila  na kusonga nusu fainali kukutana na Espaniol ambao ni mabingwa watetezi, katika nusu fainali mchezo ulimalizika kwa suluhu na Waandishi kupata ushindi kwa njia ya matuta na kusonga fainali.

Hali ilivyokua katika mchezo wa fainali kati ya Timu ya Waandishi wa Habari dhidi ya Timu ya Mkuu wa Mkoa.

Katika fainali timu ya Waandishi wa habari za michezo walikutana na timu ya Mkuu wa Mkoa na kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja katika mchezo uliokua mgumu kwa pande zote mbili lakini mwisho wa mchezo nahodha Mbwana Mshindo walifanikiwa kuibuka na ushindi na hatimae kutwaa ubingwa huo.

Kwa upande wa timu ya Wanawake ya Waandishi wa habari za michezo wao walianza safari yao kwa kuwaondoa IPP Media robo fainali na katika nusu fainali waliiondosha Spark Queens na katika fainali waliibuka vinara mbele ya Espaniola.

Nahodha wa Timu ya Mkuu wa Mkoa Thomas Mselemu akipokea zawadi ya mshindi wa pili.

Kwa kutwaa ubingwa huo timu zote mbili kwa upande wa Wanawake na wanaume walipata zawadi ya kombe na pesa taslim shilingi milioni moja ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza.

Wakati mshindi wa pili kwa upande wa wanaume ni timu ya Mkuu wa Mkoa waliopata laki tano na washindi wa tatu ni Espaniol walioweka kibindoni laki mbili na nusu.

Nahodha wa Waandishi wa Habari za Michezo Mbwana Mshindo akipokea kombe kutoka kwa Mstahiki Meya Songoro Mnyonge.

Kwa upande wa wanawake mshindi wa pili ni Espaniol walipata laki tano wakati washindi wa tatu walipata laki mbili na nusu pia.

Zawadi zote hizo zilitolewa palepale katika viwanja vya Cocobeach mbele ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Songoro Mnyonge akiambatana na watendaji wa kampuni ya Betika pamoja na Afisa habari Juvenille Lugambwa.

 

 

Sambaza....