Sambaza....

Hatimae uwanja mkongwe uliopo Jijini Mbeya unaotumiwa na klabu ya Mbeya City utafanyiwa matengenezo makubwa na wadhamini wapya wa klabu hiyo ili kukidhi vigezo vya kutumika katika michezo ya Ligi Kuu.

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch wamethibitisha hilo leo baada ya kuingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na Klabu ya Mbeya City.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika hafla fupi ya kutambulisha udhamini kati ya Parimatch na Mbeya City, afisa habari wa Parimatch Ismail Mohamed amesema wataukarabati uwanja huo ili kuendana na mahitaji ya mpira wakisasa.

Uwanja wa Sokoine.

“Mbeya City ni moja ya klabu kubwa hapa nchini yenye mashabiki wengi na ushawishi katika soka na hii ndio sababu iliyotushawishi sisi kurudi tena hapa katika msimu huu mpya. Kama mtakumbuka msimu wa 2020/2021 tulikuwa wadhamini wakuu kwa mara ya kwanza,” Ismail Mohamed.

“Parimatch pia itatoa vifaa vya michezo pamoja kufanya ukarabati mdogo katika uwanja wa Sokoine katika eneo la benchi la wachezaji ili kuufanya uwanja uwe na sifa ya kuchezewa michezo ya Ligi Kuu,” aliongeza

Nae Mtendaji mkuu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe amesema walipewa maelekezo na Bodi ya Ligi kurekebisha baadhi ya maeneo na wanasishukuru Parimatch kwa kusaidia eneo hilo.

“Tulipewa maelekezo na Bodi ya Ligi ya kurekebisha baadhi ya maeneo ya Uwanja wetu wa nyumbani (Sokoine) haswa eneo la benchi la ufundi pamoja na wachezaji. Tunawashukuru mno wenzetu wa Parimatch kwa kuweka nguvu katika eneo hilo.”

 

Klabu ya Mbeya City leo imetangaza kuingia udhamini na kampuni ya kubashiri ya Parimatch wa mwaka mmoja. Awali Parimatch waliwahi kuidhamini Mbeya City katika msimu wa mwaka 2020/2021.

Sambaza....