Sambaza....

Nusu fainali ya pili inayowakutanisha Azam vs Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha siyo nyepesi kama wengi wanavyodhani.

Azam ni timu kubwa kwa maana ya “Professionalism” lakini Coastal Union ni klabu kongwe yenye mafanikio mbalimbali na huko nyuma iliwahi kuwakilisha kimataifa kama ambayo kwa sasa wanasaka nafasi hiyo kwa njia hii.

Coastal Union inafundishwa na mchezaji wake wa zamani aliyeichezea pia timu ya Taifa Juma Mgunda. Moja ya washambuliaji nguli nyakati hizo akiwa na umbo kubwa lakini alikuwa balaa kwa kufunga kupitia mashuti yake mazito.

Wanakwenda kuchuana na Azam inayofundishwa na kocha kijana Abduhamid Moallin ambayo historia yake ya kucheza si kubwa ukifananisha na Mgunda.

Kocha wa Azam Fc Abdihamid Moalin (kulia) akielekeza jambo mazoezini.

Wote ni makocha wasiokuwa na muda mrefu ndani ya timu wanazozifundisha hasa kwa Moallin huku Mgunda akiingia na kutoka mara kwa mara kwenye timu hiyo na mara ya mwisho ilikuwa ikifundishwa na Kocha wa kigeni Melis Medo.

Coastal ya Mgunda inaonekana kufanya vyema kwa sasa hasa katika michezo mitano ya mwisho iliyochezwa ndani ya mwezi huu ameshinda 5 na kusare 1.

Tofauti na Azam katika michezo 5 ya mwisho ameshinda 2 amesare 2 na kupoteza 1 japo hii ni ya ligi kuu.

Wachezaji wa Coastal Union wakishangilia bao katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Maana yangu hapa fomu ya sasa ya Coastal ipo sawa hasa lakini hamuhakikishii kupata ushindi katika mchezo huo.

Coastal ya Mgunda kiufundi ameibadili kuanzia safu ya ulinzi iliyokuwa inawafungisha mara kwa mara chini ya Medo.

Kwa sasa ni timu nzuri inayoanzia kwenye safu ya kiungo kwenda mbele lakini safu ya ulinzi inayoongozwa na Paschal Kitenge na Jackson Shiga, Miraji Idah, Aman Kyata imekuwa na ubora mkubwa wa kucheza bila kuruhusu magoli.

Mshambuliaji wa Coastal Union Adam Uledi “Balle” akimuacha mchezaji wa Polisi Tanzania.

Burudani ya Coastal ipo kwenye idara ya kiungo inayoongozwa na Mnigeria Victor Akpan ambaye anajukumu la kupandisha mipira kwa washambuliaji hatari Abdul Sopu na Vincent Abubakar na Haji Ugando.

Hichi ndicho kinachompa kiburi kwenye formation mbalimbali anaweza kutumia 4-4-2 au 4-3-3 ama 3-5-2 ambapo Akpan ndiyo ‘high quality player’.

Azam wao kwa upande wao wamecheza tatizo kubwa lipo kwenye mlinda mlango na huwa tunasema ”nyumba ni mlango” Kigonya anaonekana kufeli na msaidizi wake hali kadhalika Ahmed Selula amefeli ilihali wamemgeukia bwana mdogo Wilbrod Maseke.

Mlinda mlango wa Azam Fc Mathias Kigonya.

Safu ya ulinzi wao nao haijawa bora hasa kwenye walinzi wa kati Agrey Morris na Abdallah Kheri Sebo wamekuwa na makosa ya mara kwa mara.

Kiungo kilichoko chini ya Kenneth Muguna na Sospeter Bajana na Mudathir Yahaya,Paul Katema Tepsie Evance wamekuwa na ubora wa juu kwa kuwa wana sifa tofauti wapo wakabaji hapo na wachezeshaji.

Keneth Muguna.

Safu wake inayoongozwa na mshambuliaji anayelijua goli vizuri Rodgers Kola ndiyo mtu wa kuchungwa sana pamoja na Charles Zulu.

Moallin pia ana option kadhaa za mifumo kwa aina ya wachezaji wake pia lakini suitable kwake ni 4-2-3-1.

Ama kwa hakika Azam yupo juu sana dhidi ya Coastal lakini itategemea maandalizi ya kisaikolojia nyenye kuongeza kuipambania timu. Mchezo huu si mzuri kwa Azam kama wataruhusu waende kwenye mikwaju ya matuta.

Sambaza....