Ligi Kuu ya NBC inaendelea tena kesho kwa mchezo mmoja ambapo wababe wa Jiji la Dar es salaam watakutana katika muendelezo wa Ligi hiyo. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa majira ya saa mbili na robo ili kuwapa mashabiki na wachezaji muda muhsusi wa kupata ftari.
Azam Fc atamkaribisha Yanga katika uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex Chamanzi katika mchezo wa raundi ya kumi na tisa wa Ligi. Tayari timu zote zimeshacheza michezo kumi na nane ya Ligi huku Yanga wakiwa kinara kwa alama zao 48 na Azam Fc wakiwa nafasi ya tatu na alama 28.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga waalibuka washindi wa mabao mawili kwa bila mbele ya Azam fc huku Yanga wakiupiga mpira mwingi katika dimba la Mkapa. Mabao ya Yanga katika mchezo huo yalifungwa na Fiston Mayele na Jesus Moloko.
Azam Fc wataingia katika mchezo wa kesho wakiwa na hamu kubwa ya kulipiza kisasi lakini pia kufuta uteja mbele ya Yanga kwa kukataa kupoteza michezo yote miwili msimu huu. Katika msimu uliopita 2020/2021 timu hizi zilitoshana nguvu wakigawana mchezo katika kila mzungunguko ambapo Yanga walipata ushindi wa bao moja bila Chamanzi kabla ya Prince Dube kuipa ushindi kama huo Azam katika dimba la Mkapa.
Azam Fc katika mchezo wa kesho watawakosa Shaban Idd Chilunda na Idd Selemani “Nado”, lakini kwa upande wa Yanga watawakosa nyota wao Deus Kaseke, Khalid Aucho, Yacouba Sogne na Feisal Salum kwasababu za majeruhi.