Sambaza....

Baada ya kutoka sare mchezo wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons klabu ya Yanga jana ilicheza mchezo wake wa pili wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbeya City .

Katika mchezo wa jana timu ya Yanga ilifanikiwa kushinda kwa goli moja kwa bila (1-0) goli lililofungwa na Lamine Moro baada ya kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Carlinhos.

Baada ya mchezo huo mjumbe wa kamati ya usajili wa Yanga , Injia Hersi Said amedai kuwa taratibu timu imeanza kuunganika.

“Taratibu timu imeanza kuunganika. Tuna kikosi kikubwa leo atacheza huyu kesho atacheza huyu. Kwa hiyo timu inaanza kuunganika taratibu “- alisema Injinia Hersi.

Kuhusu kucheza kwa Carlinhos , Injinia Hersi Said amedai kuwa Carlinhos alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwa hiyo taratibu anaanza kuzoea.

“Carlinhos alikuwa hajacheza kwa kipindi kirefu kutokana na ugonjwa wa Covid-19. Ameanza kupewa dakika za kucheza. Leo kapewa dakika 30, kesho dakika 45 kuna siku atapewa dakika 90”.

Kuhusu malengo ya Yanga msimu huu , Injinia Hersi Said aliuambia mtandao huu wa kandanda.co.tz kuwa lengo lao ni kuchukua ubingwa tu.

“Lengo letu kwa sasa ni kuchukua ubingwa tu na siyo kitu kingine. Wachezaji tunawapa Bonus zao tangu mechi ya kwanza , tunalenga kuchukua ubingwa msimu huu”- alimalizia Injia Hersi Said

Sambaza....