Sambaza....

Jana timu ya wananchi (Yanga) ilifanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya kuwafunga Mbeya City katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya mchezo huo mtandao wa Kandanda.co.tz ulifanikiwa kuzungumza na aliyewahi kuwa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba , Senzo Mbatha.

Senzo Mbwatha alidai kuwa mji wa Roma haukujengwa siku moja hivo timu yao inajengeka taratibu hivo mashabiki wawe na utulivu.

“Timu yetu inajengeka taratibu kila siku kuna mabadiliko kwenye timu yetu hivo uvumilivu unahitajika kwa sababu hata Roma haukujengwa ndani ya siku moja”- alisema Senzo Mbatha.

Senzo Mbatha pia alisifia usajili ambao umefanyika katika timu ya Yanga kwa kusema ni usajili bora ambao utainufaisha timu ya Yanga.

“Tunatakiwa kuijenga taratibu timu yetu na njia pekee ya kuijenga taratibu ni kufanya kazi mazoezini , kufanya kazi mazoezi kila siku. Tuna wachezaji wazuri ndani ya kikosi cha Yanga ” – alidai Senzo.

Kuhusu timu ya Yanga kuhamia Kigamboni kwa ajili ya kuweka kambi na kufanyia mazoezi Kigamboni badala ya uwanja wa sheria pale Ubungo wazo ambalo alitoa yeye Senzo amedai kuwa anachoshukuru Yanga haiendeshwi na mtu mmoja.

“Yanga haiendeshwi na mtu mmoja , kuna mwenyekiti wa klabu Dkt. Mshindo Msolla , wajumbe wa kamati tendaji , wadhamini wetu. Nashukuru walikubali ombi la kuhamisha kambi. Kambi ni ya gharama lakini ndicho kitu ambacho kinahitajika”- alimalizia Senzo Mbatha.

Sambaza....