Sambaza....

Jana ilikuwa siku ya furaha kwa wananchi mara baada ya mchezaji wao pendwa Carlinhos kuonesha kiwango kikubwa kwenye mechi dhidi ya Mbeya City.

Baada ya mechi hiyo kocha mkuu wa klabu ya Yanga alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchezo huo.

Moja ya swali ambalo aliulizwa na waandishi wa habari ni kwanini hakumwanzisha Carlinhos katika mchezo huo dhidi ya Mbeya City.

Kocha huyu alidai kuwa hawezi kumua Carlinhos kwa kumpa dakika nyingi za kucheza kwa sababu hajacheza kwa muda mrefu.

“Carlinhos na Yacoub Sogne hawajacheza kwa miezi mitano. Ligi zao zilikuwa zimefungwa kwa sababu ya ugonjwa wa covid-19. Kwa hiyo siwezi kumwanzisha dakika nyingi”.

“Taratibu nawapa muda. Ni ngumu kwa mchezaji ambaye hakucheza miezi mitano kumpa muda mwingi wa kucheza. Kwa hiyo siwezi kumua mchezaji wangu kwa sasa”- alimalizia kocha huyo mkuu wa Yanga.

Sambaza....