Ikiwa imebaki siku moja kufikia kilele cha siku ya Wananchi itakayofanyika siku ya kesho Jumapili 30 August katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam mashabiki wa Yanga wasubiri utambulisho wa majina makubwa klabuni kwao.
Licha ya uwepo wa wasanii wakubwa nchini kama Harmonise, G nako, Juma Nature na Msaga Sumu lakini burudani itabaki palepale katika mpira wa miguu ambao mashabiki wa Yanga wanasubiri kuwaona nyota wao kwa mara ya kwanza.
Kabla ya kucheza mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa dhidi ya mabingwa wa Burundi Aigle Noir Yanga itawatambulisha nyota wake wapya watakaowatumia katika msimu wa 2020/2021.
Nyota watakaotambulishwa kesho:
Walinda Mlango
Farouk Shikalo (Kenya)
Metacha Mnata
Ramadhan Kabwili
Walinzi wa Kati
Lamine Moro (Ghana)
Said Juma Makapu
Abdallah Shaibu Ninja
Bakari Nondo Mwamnyeto
Walinzi wa pembeni
Paul Godfrey “Boxer”
Kibwana Shomari Yasin Mustapha
Adeyoun Saleh
Viungo Wakabaji
Feisal Salum Abdallah “Fei Toto”
Abdulaziz Makame “Bui”
Zawadi “Gift” Mauya
Mukoko Tonombe (DR Congo)
Viungo Washambuliaji
Balama Mapinduzi “Kipenseli” Haruna Niyonzima (Rwanda)
Deus Kaseke Juma Mahadhi
Tuinsila Kisinda (DRC Congo)
Farid Mussa Carlinhos (Angola)
Washambuliaji
Michael Sarpong (Ghana)
Waziri Junior
Ditram Nchimbi