Msimu wa mwaka 2018/2019 ndiyo msimu ambayo mtandao wa www.kandanda.co.tz ulianzisha bidhaa yake ya Galacha wa magoli. Bidhaa ambayo ililenga kusherehekea kwa pamoja na wafungaji bora wa kila mwezi kwenye ligi kuu.
Mtandao wa kandanda.co.tz umefanikiwa kutoa zawadi kwa wachezaji mbalimbali wa ligi kuu Tanzania bara kwa misimu miwili mfululizo. Msimu wa mwaka 2018/2019 na msimu wa mwaka 2019/2020.
Misimu ambayo ilikuwa yenye mafanikio makubwa sana ambapo kila mchezaji ambaye alifanikiwa kuwa mfungaji bora wa mwezi husika alipewa zawadi ya kiatu kutoka kandanda.co.tz kama sehemu ya kusherehekea naye kwa pamoja mafanikio yake ya mwezi husika.
Msimu wa mwaka 2019/2020 kandanda.co.tz ilipata ubia na Mgahawa Cafe & Restaurant ambao wapo mtaa wa OHIO kwenye jengo la Golden Jubilee Tower. Mgahawa Cafe na Kandanda.co.tz kwa pamoja waliongeza thamani kwenye bidhaa hii ya GALACHA WA MAGOLI.
“Tulifurahi sana kufanya kazi na Kandanda, zaidi ni kuleta uhusiano wa chakula na Mpira wa miguu“. Bi Fatma Dahir, mmiliki wa Mgahawa Cafe & Restaurant. ” Huduma zetu za chakula na vinywaji vinatia nguvu hata kwa wasukuma kandanda, na mtandao huu umetusogeza karibu na wadau wa mpira wa miguu zaidi.” aliongeza mmiliki huyo.
Mgahawa Cafe & Restaurant wanaandaa Chakula katika mazingira ya kumtosheleza mchezaji pia ambaye anahitaji virutubisho bora kwaajili ya kujenga afya na utimamu wa mwili na akili, na hata wale wateja ambao kila asubuhi wanapita pale kupata vifungua kinywa, mchana kupitia kupata mlo wa mchana na jioni au muda wowote kwa wapenzi wa kahawa na chai.
FAIDA ALIZOZIPATA MGAHAWA CAFE & RESTAURANT
1Bidhaa yake ya Mgahawa Cafe ilipata nafasi kubwa ya kuonekana kwa watu wengi kwa sababu alipata nafasi ya kutangazwa kwenye mtandao wa kandanda.co.tz pamoja na kurasa za mitandao ya kijamii ya Kandanda. (Facebook , Twitter na Instagram ).
2Mgahawa Cafe alipata nafasi kubwa ya kuongeza mauzo yake kutokana na yeye bidhaa yake kuonekana sehemu kubwa.
3Chapa yake ya Mgahawa Cafe ilipata nafasi ya kuaminika zaidi na zaidi kwa sababu ilikuwa inajihusisha na watu wenye ushawishi kwenye mpira wa miguu (Influencers ).
Kandanda.co.tz bado inaendelea kuwakaribisha wadau wengine ambao watashirikiana na mtandao nasi katika utoaji wa tuzo ya Galacha wa magoli kwa msimu 2020/2021. Lengo letu likiwa ni kuboresha kila msimu.
Msimu wa 2019/2020 umemalizika kwa kushuhudia Meddie Kagere akiwa ndiye mfungaji bora wa msimu huo akiwa na magoli 22. Hivyo kandanda.co.tz inasherehekea naye kwa pamoja katika mafanikio yake makubwa ya msimu uliopita ikimtambua kama Galacha wa magoli wa msimu, akiwa anapokea tuzo hiyo kwa msimu wa pili mfululizo.
Mtandao wetu unatumia takwimu husika zinazokusanywa katika mtandao wetu, takwimu hizo zinatumika katika kusheherekea na wachezaji wanaofanya vizuri uwanjani.
Baada ya misimu miwili ya mafanikio, katika msimu wa 2019/20 tumefanikiwa kutoa Tuzo kwa Timu Galacha ya Msimu (Simba Sc), Galacha wa Hat-trick (Obrey Chirwa, Azam FC) na kumalizia Galacha wa Magoli wa Msimu (Meddie Kagere, Simba SC)