Aliyewahi kuwa mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Simba Senzo Mbatha amerudi Tanzania akitokea nyumbani kwao Afrika kusini.
Mtandao huu ulikuwepo uwanja wa Taifa pamoja na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kumpokea Senzo Mbatha.
Senzo Mbatha anaenda kuwa mkurugenzi mtendaji kivuli wa klabu ya Yanga. Alipoulizwa anachukuliaje kitendo cha kuhamia Yanga kutokea Simba, Senzo Mbatha amedai kuwa ni uamuzi wa kushangaza.
“Najua watu watajiuliza sana kwanini nimeenda kwenye klabu ambayo haijafanya vizuri ndani ya misimu mitatu iliyopita. Wote tunafahamu kuwa Yanga ndani ya misimu mitatu iliyopita haijachukua kombe”.
“Simba imeshapiga hatua kwenye suala la uendeshaji wa timu ukilinganisha na Yanga. Naenda kwenye timu ambayo tunatakiwa kuijenga upya”.
“Naamini mimi, mwenyekiti wa klabu na GSM tutashirikiana kwa pamoja kuijenga klabu mpya na hapa ndipo uwezo wangu utakapoonekana zaidi”.
“Tunahitaji benchi imara la ufundi, wachezaji bora na uongozi imara wa klabu ili kuibalidilisha klabu hii” – alimalizia Senzo Mbatha