Sambaza....

Klabu ya soka ya Azam FC imeamua kuachana na golikipa wa kimataifa kutoka Ghana , Razack Abalora. Golikipa huyo amedumu na kikosi hicho kwa muda wa misimu mitatu huku akiidakia Azam FC kwa kiwango kikubwa.

Katika nyakati zake wakati akiwa Azam FC aliiwezesha Azam FC kushinda kombe la Kagame Cup , Mapinduzi Cup pamoja na kombe la Azam Federation Cup kombe ambalo liliwapa nafasi Azam FC kushiriki kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika msimu uliopita.

Sambaza....