Sambaza....

Tayari Simba amenyakua ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku wakibaki Yanga, Azam fc na Namungo wakitafuta ni nani atakaefuata katika nafasi yapili na ya tatu. Lakini pia kule chini kuna mbio za timu kama nane zinazopambana kutokushuka daraja.

Baada ya Simba kupata tiketi ya kushiriki michuaono ya Ligi ya Mabingwa Afrika  kwa kuibuka Bingwa wa Ligi msimu huu tiketi moja pekee imebaki katika ushiriki wa michuano ya Kimataifa nayo ni kupitia Azam Sports Federation Cup (Kombe la FA).

Yanga kwa upande wao wanaitazama nafasi hii kama sehemu muhimu ya kuendelea kujenga kikosi kijacho katika msimu ujao lakini pia kuirudisha timu katika mstari mbele ya mashabiki wao kuelekea katika mabadiliko ya klabu kwenye umiliki.

David Molinga na Mrisho Ngassa wakishangilia goli katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Njia pekee iliyobaki ya Yanga kuweza kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao ni kuifunga Simba katika nusu fainali na pia kuifunga Sahare All Star au Namungo katika mchezo wa fainali ili waweze kuiwakilisha nchi katika michuano ya Shirikisho Afrika.

Lakini kizingiti kikubwa ambacho Yanga wanakiona mbele yao ni Simbsc ambao wanakwenda kukutana nao kwa mara ya tatu msimu huu siku ya Jumapili. Nikama tiketi yao imeshikiliwa na Simba, Siimba wao walishakula kiapo na kuonyesha nia ya kuhitaji kubeba makombe yote msimu huu likiwemo la FA.

Papy Kabamba Tshishimbi akiwa katikati dhidi ya wachezaji wa Township Rollers ya Botswana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ni wazi msimu huu Yanga haikua na umakini na bahati pia katika usajili haswa wa nyota wa Kimataifa. Hivyo kupitia GSM kama mfadhili mkuu wa Yanga tayari wameapa kukisuka upya kikosi chao kwa kushusha nyota wa Kimataifa wa maana watakaoendana na hadhi ya Yanga.

Lakini ili kuwapata na kuwavutia nyota wakubwa Afrika ni lazima timu iwe inashiriki michuano ya Kimataifa na kocha Mkuu wa Yanga Luc Aymael analijua hilo.

Luc Eymael, Kocha wa Yanga sc

Hivyo nusu fainali hii kwa Yanga ni kama itaamua hatma ya klabu yao kwa msimu ujao. Wanahitaji tiketi ya kuiwakilisha nchi Kimataifa ili kwenda sawa na presha ya Simba lakini pia wanahitaji nafasi hiyo ili kuweza kuwashawishi nyota wakubwa Barani Afrika kujiunga nao, kwa maaana mchezaji mkubwa anapenda kushiriki michuano mikubwa.

Sambaza....