Sambaza....

Nusu fainali ya kombe la Azam Federation Cup ishajulikana ni nani atakutana na nani . Namungo FC ambao wamepanda daraja msimu huu wanaenda kukutana na Sahare All Stars timu ya daraja la kwanza.

Mechi kubwa ya nusu fainali ambayo itateka hisia za watu wengi ni kati ya Simba na Yanga , mechi ya watani wa jadi. Mechi ambayo inazikutanisha timu ambazo zina mashabiki wengi nchini.

Ditram Nchimbi akimkimbiza mlinzi wa Simba Tairone Santos.

Tuachane na habari za wao kuwa na mashabiki wengi . Tuzitazame timu hizi tatu ambazo zinaonekana ndizo timu kubwa hapa nchini yani Azam FC , Simba na Yanga . Ipi ni timu bora kuzidi zote ?

ENEO LA ULINZI

Kwenye eneo hili Simba kwa msimu huu wamekuwa imara zaidi kuzidi Yanga na Azam FC. Mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Tanzania bara, Simba amefungwa magoli 16 , Azam Fc wakiwa wamefungwa magoli 23 na Yanga wakiwa wamefungwa magoli 25 mpaka sasa hivi. Takwimu hizi zinaibeba Simba kama timu imara kwenye eneo hili la ulinzi kuzidi Azam FC na Yanga.

Pascal Wawa akimthibiti Richard Djodi wa Azam fc

ENEO LA KIUNGO CHA KATI

Simba ina utajiri mkubwa wa viungo wa kati kuzidi Azam FC na Yanga . Viungo ambao wanauwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za magoli kuzidi viungo wa Azam FC na Yanga . Pamoja na kwamba viungo hawa wanauwezo wa kutengeneza nafasi za magoli lakini viungo hawa wanauwezo unakaribiana , viungo wa kati wa Simba wanaokaa benchi wanakaribiana kwa kiasi kikubwa na viungo ambao wapo uwanjani tofauti kabisa na viungo wa Yanga na Azam FC.

Sharaf Eldin Shiboub akiwa dimbani

ENEO LA KUSHAMBULIA

Hili ni eneo ambalo linabeba uhatari wa Simba kwa kiasi kikubwa. Simba msimu huu kwenye ligi kuu Tanzania bara wamefunga magoli 69 , Azam FC wakiwa wamefunga magoli 41 na Yanga wakifunga magoli 38. Kitu ambacho kinaonesha kuwa Simba wana safu imara ya ushambuliaji kuzidi Azam FC na Yanga.

Kwa hiyo ukitazama maeneo yote ya uwanja , Simba inaonekana imara kuzidi Azam FC na Yanga ambao wanaonekana ni wapinzani wakubwa kwenye ligi kuu ya Tanzania bara.

Sambaza....