Baada ya Ligi Kuu Bara kutangazwa kurejea kama kawaida baada ya kusimamishwa kutokana na virusi vya ugonjwa wa corona tayari baadhi ya wachezaji na makocha wa kigeni wameanza kurejea nchini ili kutumikia klabu zao.
Kocha mkuu wa klabu ya Azam fc Mromania Aristica Ciaoba ni miongoni mwa makocha walioondoka nchini na kwenda nchini kwao ili kupisha ugonjwa wa corona uliosababisha kwa Ligi kusimama. Lakini ilikua ni mtihani mkubwa kwake kurejea nchini baada ya Mh. Rais John Magufuli kutangaza kurejea kwa shughuli za michezo kama kawaida kuanzia June 1.
Msemaji wa Azam fc Zaka za kazi amefichua ni jinsi gani kocha huyo ilimuwia wakati mgumu mpaka kuweza kufika nchini. Huku akisema kocha wao alipanda mpaka lori la mizigo ili lifanikisha safari yake.
Zakaria “Kocha wetu alikua Romania na bado marufuku ya kutoka nje ipo nchini kwao na pia mipaka bado imefungwa. Kwa Romania nchi jirani zote pia mipaka imefungwa mpaka Ujerumani ndio wao wamefungua anga yao lakini malori ya mizigo ndio yanaruhusiwa kusafiri huku wakiwa na watu wachache.
Ilibidi apande lori kutoka Romania kupitia Hungary halafu akapitia Austria ndipo akaingia Ujerumani utaona kuna nchi mbili kabla ya kufika Ujerumani kupanda ndege. Ilimgharimu saa 23 njiani ni saa nyingi ametumia njiani lakini ni jambo la kheri amefika.”
Wakati wote huo wa safari kocha Aristica Cioaba alikua pamoja na kocha wa viungo pia wa Azam fc ambae pia ni Mromani Costan Birsan.