Ligi kuu Tanzania bara inatarajia kuanza mapema mwezi huu baada ya kusimama kipindi kirefu kutoka na janga la Covid-19 . Timu mbalimbali zimeanza maandilizi kwa ajili ya kurejea kwenye ligi. Moja ya timu hiyo ni Yanga SC.
Ambapo jana Yanga SC walifanya vipimo mbalimbali kwa wachezaji wao kwa ajili ya kujiandaa na ligi kuu Tanzania bara. Kwa mujibu wa daktari mkuu wa timu ya Yanga , hakuna mchezaji wa Yanga ambaye amepatikana na virusi vya Corona .
“Kwanza namshukuru Mungu mpaka sasa hivi hakuna mchezaji ambaye amekutwa na virusi vya corona vinavyosababisha Covid-19, wachezaji wote tumewapima na tumewakuta wako salama na hakuna mwenye maambukizi”-alisema daktari mkuu wa Yanga.
Daktari huyo pia ameelezea kuwa kwa sasa wachezaji wanaendelea na mazoezi ila wanafanya kwa tahadhali sana kwa sasa pamoja na kwamba wamefanyiwa vipimo na kugundulika kuwa hawana virusi vya Corona vinavyosababisha Covid-19.
“Tunachukua tahadhali kubwa kwa sasa mazoezini pamoja na kwamba hakuna mchezaji ambaye amekutwa na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19”-alisema daktari huyo mkuu wa Yanga .
Daktari huyo pia amedai kuwa kwa sasa wachezaji watakuwa wanafanya mazoezi huku wakiwa na masks (barakoa) , gloves na huku wakiwa wanatumia vitakasa mikono kabla na baada ya mazoezi.
“Mazoezini wachezaji watakuwa na barakoa kila mmoja , gloves pamoja na vitakasa mikono yani Sanitizer. Pia wachezaji watakuwa wana nawa kwa maji yanayotiririka pamoja na sabuni huku mipira ambayo inatumika mazoezini itakuwa inapuliziwa sanitizer”- alimalizia daktari huyo wa Yanga