Sambaza....

Tayari bodi ya Ligi kupitia kikao kilichofanywa Jumapili wamekubaliana kumalizia raundi 10 za VPL zilizobaki kutokana na ugonjwa wa corona uliopelekea serikali kusimamisha shughuli zote zinazohusisha mikusanyiko ya watu.

TPBL inapendekeza katikati ya mwezi June Ligi ianze kuchezwa bila ya mashabiki huku pia ikuhudhuriwa na maofisa wachache na waandishi wa habari wachache kukiwa na tahadhari kubwa miongoni mwa timu shiriki. Lakini mapendekezo yote hayo yatategemea ruhusa ya serikali na hatua za kufuatwa kutoka kwa wizara zote husika.

Ikiwa Ligi itarejea kama kawaida baadhi ya timu za Ligi  Kuu Bara ambazo zinamiliki wachezaji wa kigeni huenda zikapata tabu kutokana na baadhi ya makocha na wachezaji kutimka nchini na kwenda nchini kwao kujiunga na familia zao.

Kocha wa Yanga Luc Aymael (kushoto) na kocha wa Simba Sven Van Debroek.

Kuna wachezaji na makocha wanaotoka nchi kama Ubeligiji, Burundi, Zimbabwe, Ghana, Msumbiji, Zambia, Uganda, Kenya na Rwanda ambazo katika nchi zao mipaka imefungwa ili kuzuia muingiliano wa watu ili kuthibiti ugonjwa wa corona.

Hivyo hata wakirudi nchini watachelewa kujiunga na wenzao moja kwa moja kutokana na kutakiwa kukaa kwa siku 14 karantini ili kuchekiwa kama hawana maambulizi ya virusi vya corona. Kutokana na athari hizo tazama nyota ambao huenda wakakosekana katika vikosi vyao.

Azam fc itawakosa

 Bruce Kangwa, Donald Ngoma – Zimbabwe

 Razack Barola, Yakubu Mohamed, Asamoah – Ghana

Nicholaus Wadada  Uganda

Kocha Mkuu Aristica Cioaba

Nicholaus Wadada wa Azam fc raia wa Uganda akijaribu kumzuia Keneth Masumbuko wa Lipuli fc.

Simba sc itawakosa 

Meddie Kagere – Rwanda                               

Francis Kahata – Kenya                                 

Luis Miquissone – Msumbuji                         

Clatous Chama – Zambia                             

  Sharaf Shiboub – Sudan

Meddie akiwa katika mazoezi

Yanga itawakosa

Kocha Mkuu Luc Aiymael.                         

Benard Morisson – Ghana

Luc Aymael kocha mkuu wa Yanga sc.

Si hizo timu tatu tuu ambazo zitaathirika lakini pia hata “Kino Boys” nao huenda wakawakosa baadhi ya nyota wao wanaotokea Burundi Jonathan Nahimana na Emmanuel Mvuyekure

Sambaza....