James Msuva mshambuliaji wa KMC “Kino boys” ametoa ya moyoni kuhusiana na mlipuko wa ugonjwa ambao umepelekea kusimamishwa kwa Ligi Kuu Bara kwa hapa nchini lakini pia Ligi kubwa barani Ulaya pia zikiwa zimesimama.
Mchezaji huyo wa zamani wa Mbao fc na Yanga amesema kama wachezaji hawajaathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na Ligi kusimama ili kuzuia maambukizi ya corona lakini pia hakusita kuzungumzia familia na nchi kwa ujumla.
James Msuva “Kwa timu tulikuwa na muendelezo mzuri (baada ya kushinda michezo minne mfululizo) lakini kwasasa tunapata muda wa wakujiandaa zaidi.
Kwangu kawaida tu maana nazingatia yote yaliyosemwa na wataalam wa Afya, lakini pia ni lazima uwe na hofu kwa familia na nchi kwa ujumla.”
Lakini pia hakusita kuelezea mapumziko haya yeye kama mchezaji jinsi ya kujilinda ili kurudi katika Ligi wakiwa imara kabisa.
Msuva “Kujilinda ni kufanya mazoezi zaidi maana Ligi bado haijaisha ni imesimama tuu kwa muda. Sidhani kama kutaathiri (kama KMC) naimani tutarudi vizuri zaidi kwa uwezo wa Mungu.”