Sambaza....

Achana na mechi ya Watani iliyobakisha siku 4 tu kupigwa pale Kwa Mkapa, achana na matokeo mazuri wanayoyapata Simba sc kwa sasa katika michezo mitano mfululizo tazama jinsi Simba inavyocheza mpira safi uwanjani.

Msemaji wa klabu ya Simba Hajji Manara aliwahi kunukuliwa akisema wataongea na mamlaka zinazohusika wajaribu kuongeza kiingilio katika mechi za Simba. Akiwa na maana kua pesa ya kiingilio ni ndogo na haifanani na thamani ya kiwango wanachocheza wachezaji wa Simba.

Haji Manara msemaji wa klabu ya Simba

Katika miaka ya 1980 ilitokea pale uwanja wa nyumbani wa Ajax katika mchezo mmoja wa Ligi nchini Uholanzi, kuna shabiki mmoja aliondoka uwanjani wakati wa mapumziko akisema anawadhulumu wachezaji. Shabiki huyo alidai kiingilio alichotoa hakifanani na burudani anayoipata kutokana na wachezaji wa Ajax wanavyotandaza soka safi.

Alienda mbali zaidi na kusema kiasi cha fedha alicholipa kama kiingilio ni kidogo hivyo ni vyema aongeze tena kiasi cha fedha au aamue kuondoka uwanjani wakati wa mapumziko maana kuendelea kuwepo uwanjani ni kuwakosea wachezaji

Mashabiki wakifwatilia mchezo wa timu yao katika uwanja wa Taifa.

Katika Ligi Kuu Bara kuna hii Simba Sports Club ambayo inashinda na inaburudisha uwanjani kwa namna ambavyo wanatandaza soka safi kabisa. Simba hii inacheza kwa kasi, utulivu na ufundi wa hali ya juu na hii ni kutokana na kuwa na wachezaji mmoja mmoja wenye uwezo mkubwa.

Katika mchezo dhidi ya Azam fc Simba imeshinda mabao matatu kwa mawili, achana na matokeo itazame Simba ilivyokua inacheza uwanjani kuanzia nyuma mpaka mpira unapofika katika eneo la timu mpinzani haswa katika eneo la hatari.

Jonas Mkude akicheza kweli kama kiungo wa ulinzi anauamrisha mchezo na hivyo kuwapa urahisi viungo wa juu yake kupokea mipira na kuweza kuanzisha hatari kwa mpinzani. Yeye anakua mtu muhimu haswa katika mfumo wa 4:1:4:1 au 4:1:3:2.

Jonas Gerad Mkude

Kuna huyu Cleotus Chama ana kila kitu cha kumfanya aitwe kiungo wa ushambuliaji. Licha ya kupika mabao mawili kipindi cha kwanza lakini amefanya viungo wa Azam Bryson Raphael na Sure Boy wazurure uwanjani haswa katika kipindi cha kwanza.

Halafu kuna hawa watu Deo Kanda, Francis Kahata ni wachezahi halisi wa kiungo wa pembeni. Wanajua kumfanya beki wa timu pinzani awe “busy” na wao na kushindwa kusaidia mashambulizi kama ambavyo Bruce Kangwa na Nicholaus Wadada leo wamekiona cha moto.

Deo Kanda akiifungia Simba katika mchezo dhidi ya Azam fc.

“Konde Boy” Luis Miquissone kasheshe nyingine hii ndani ya kikosi cha Simba, kipi kingine hajafanya kama kiungo wa ushambuliaji? Akitokea pembeni hatari, akitokea katikati nyuma ya mshambuliaji ndio hatari zaidi. Luis ameongeza ubunifu katika eneo la ushambuliaji akiongeza utengenezaji wa nafasi na kutoa msaada wa mabao kwa washambuliaji wa Simba.

Luis Miquissone, Francis Kahata, Cleotus Chama na  Deo Kanda leo wamefanikiwa kurudisha viingilio vya wapenzi watazamani waliojitokeza leo katika mchezo wao dhidi ya Azam kwa burudani za hali ya juu.

 

Cheng

Wachezaji wa Simba walishangilia goli lao dhidi ya Azam fc

a za maudhi, pasi za kugongeana za haraka mpaka kwenye box  na kasi ya hali ya juu vimewafanya mashabiki wa Simba waondoke uwanjani  wakiwa na furaha mara mbili. Furaha ya matokeo na furaha ya soka safi.

Utamu wote huo ukahitimishwa na magoli saafi ya Erasto Nyoni, Deo Kanda na Meddie Kagere.

 

Sambaza....