Jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kulikuwa na mechi ya ligi kuu Tanzania bara kati ya Tanzania Prisons na Yanga , mechi ambayo ilimalizika kwa suluhu.
Mechi ambayo ilishuhudiwa na mtandao huu wa kandanda.co.tz , na baada ya mechi hii kocha wa Yanga alizungumza na vyombo vya habari ikiwemo Kandanda.co.tz
Kocha huyo alidai kuwa Kwa sasa wanawatazama sana Azam FC ambao ndiyo washindani wao katika nafasi ya pili ambao jana walifungwa dhidi ya Coastal Union magoli 2-1.
“Tunaangalia namna ya kushika nafasi ya pili kwa sasa , tunawatazama Azam FC ambaye amefungwa . Lengo letu ni kushika nafasi mbili za juu”-alidai Luc Eymael.
Kuhusu ratiba amedai kuwa ratiba kwao kwa sasa ni ngumu haiwapi muda wa kupumzika , wachezaji wanacheza mfululizo.
“Tumewapumzisha wachezaji takribani wa nne kama Jafarry , Niyonzima ambaye alikuwa anaumwa malaria , Golikipa pamoja na Ditram Nchimbi ”
“Tulimweka Tariq eneo la pembeni tukiamini anavyopigana angeisaidia timu na pia wengi walikuwa wanauliza kuhusu Mohamed Banka tumempa nafasi Leo mnaweza mkatoa maoni yenu kuhusu kiwango chake “alisema Kocha huyo wa Yanga
Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa timu kusafiri na Haruna Niyonzima kwenda Moshi amedai kuwa Haruna Niyonzima amemuomba kusafiri naye Lakini wataangalia kama atacheza
“Tunasafiri kuelekea Moshi ambapo tuna mechi jumanne , Haruna Niyonzima ameniomba awe sehemu ya timu itakayosafiri kwenda Moshi”- alimalizia kocha huyo wa Yanga