Sambaza....

Jana kulikuwepo na mchezo kati ya Yanga na Mbaya City katika uwanja wa Taifa . Mchezo ambao ulichezwa siku ambayo Yanga ilikuwa inasherehekea miaka 85 tangu ianzishwe.

Mechi hiyo ilimalizika kwa timu zote kutoka sare ya goli moja kwa moja , goli la Mbeya City lilipatikana baada ya beki wa Yanga , Lamine Moro kujifunga huku goli la Yanga lilipatikana baada ya Bernard Morrison kufunga kwa kichwa.

Ditram Nchimbi “Duma” akiwa mazoezini na klabu yake ya Yanga.

Baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael amedai kuwa timu yake imekuwa ikionewa na waamuzi kwa sababu hii ni mara ya pili kwa timu yake kunyimwa goli.

“Nafikiri Leo timu yangu ilistahili kupata penati , nitaenda kutazama kwenye TV. Mechi iliyopita dhidi ya Ruvu Shooting tulinyimwa penalti baada ya Bernard Morrison kuangushwa eneo la hatari , na leo kuna penati tumenyimwa pia”-alidai kocha huyo kutoka Ubelgiji.

Luc Eymael, Kocha wa Yanga akiongea kabla ya mechi

Kocha huyo pia amedai kuwa ndiyo maana waamuzi wengi wa hapa hawachaguliwi kwenda kuchezesha michuano mikubwa kama michuano ya Afcon kwa sababu ya kiwango kibovu .

“Niwaulizeni ni mwamuzi yupi alienda kucheza mashindano ya Afcon ?, hakuna ?, Asante kwa hilo”. alimalizia kocha huyo mkuu wa Yanga

Sambaza....