Sambaza....

Simba wameshaachana na Patrick Aussems , Ndoa yao kwa sasa haina uhai, ila kwa sasa kuna penzi jipya Kati ya Simba na kocha wao mpya Sven Vandenbroeck. Haya ni mambo matatu ambayo unatakiwa kuyafahamu kuhusu kocha huyu.

RAIA WA UBELGIJI

Kama ilivyokuwa kwa Patrick Aussems kutoka katika nchi ya Ubelgiji ndivyo ilivyo kwa Sven Vandenbroeck ambaye pia ni RAIA wa Ubelgiji na amezaliwa mwaka 1979 kwa sasa ana umri wa miaka 40. Katika maisha yake ya mpira amewahi kucheza katika nafasi ya kiungo wa kati.

UKOCHA

Katika ngazi ya ukocha Sven Vandenbroeck amefanikiwa kuitumikia Niki Volou kama kocha wao, pia aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Cameroon 2017, Cameroon ambayo ilichukua Afcon 2017. Baada ya kufanikiwa kuchukua Afcon akiwa kama Kocha msaidizi , mwaka 2018 alichaguliwa kuwa kocha wa Zambia. Alidumu kwa miezi tisa (9) tu na Zambia walishindwa kumuongezea mkataba Baada ya kushindwa kuivusha Zambia kwenda Afcon 2019.

UKOROFI

Hii ni tabia ambayo imezungumzwa sana na waandishi wa Habari wa Zambia. Baada ya kutangazwa kuwa kocha mkuu wa Simba , baadhi ya waandishi wa Habari wa Zambia waliuambia mtandao huu kuwa kocha huyu ni kocha Mkorofi sana, kuna wakati huwa anakuwa na hasira za karibu wakitolea mfano kitendo cha kuwa na hasira kipindi anatangaza kikosi cha Zambia Baada ya kuanza kuulizwa maswali. Pia Wametahadharisha kuwa kocha huyu hana uwezo wa kuvumilia presha ya Simba.

Sambaza....