Baada ya Simba kuachana na aliyekuwa kocha wao mkuu, Patrick Aussems, kituo cha radio cha AFM kilichopo jijini Dodoma kilifanya mahojiano na kocha huyo ambaye kwa sasa yupo na familia yake kapumzika.
Kocha huyo aliwashukuru wachezaji wa timu hiyo na mashabiki wa timu hiyo. “Kwanza kabisa napenda kuwashukuru wachezaji kwa kazi ambayo tumefanya kwa pamoja ilikuwa kazi kubwa. Pia napenda kuwashukuru mashabiki wa timu, nimepata ujumbe Mwingi kutoka kwa mashabiki”.
Alipoulizwa kwanini amefukuzwa na Simba. Alisema kuwa kuna vitu vingi vikubwa ambavyo vilikuwa vinatokea kwenye bodi ya Simba. Kuna wanabodi Wa Simba ambao hawaendi kwenye njia sahihi hawaendi kwenye maono na Mo , walikuwa wanamwambia Mo kuwa siwezi kuwa kocha bora.
Alipoulizwa kuwa maneno yanayosemwa amefukuzwa kwa sababu ya kushindwa kufikia malengo ya Simba. Alisema kuwa walikuwa na malengo ya pamoja ya kufika kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa , lakini kwa bahati Mbaya walitolewa , walipotolewa ilibidi kufikiria namna ya kufanya vizuri kwenye michuano ya ndani na ndicho walichokuwa wamefanikiwa.
Kuhusu yeye kuhusika moja kwa moja kwenye usajili alikataa , yeye alitaka wachezaji baadhi wabaki kama kina Emmanuel Okwi, James Kotei. Lakini viongozi walishindwa na kusajili wachezaji wao.
Kuhusu ligi yetu amedai kuwa ligi yetu ya kawaida kwa sababu ina timu tatu tu Azam FC, Simba na Yanga ambazo ni kubwa. Zingine ni za kawaida na zinacheza katika viwanja vibovu vyenye eneo la kuchezea bovu.