Kwa Mara ya kwanza baada ya miaka kumi Tanzania ilifuzu kucheza michuano ya CHAN ikiwa ni Mara ya pili. Tanzania iliifunga Sudan magoli 2-1 na kufanikiwa kufuzu kwa faida ya goli la ugenini baada ya mchezo wa kwanza kufungwa 1-0 kwenye uwanja wa Taifa.
Kwenye mchezo wa jana Ditram Nchimbi alisababisha faulo iliyozaa goli , pia alifunga goli la ushindi . Kabla ya mchezo huo Ditram Nchimbi aliongezwa katika dakika za mwisho kwenye kikosi cha timu ya Taifa na kasababisha maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii.
“Nilikuwa naona kwa sababu na mimi niko kwenye mitandao Nilijisikia kawaida tu wala haikunivunja moyo, Lakini Mimi nafahamu Sisi Watanzania Tulivyo Mimi mwenyewe Ni Mtanzania na Sisi Watanzania Tunajuana hatuwezi kuamini mpaka Tuone au Tushuhudie mtu kafanya Kitu Fulani na mpaka Mtanzania akubali kazi yako sio Mchezo kumuaminisha Mbongo ” amesema Ditram Nchimbi
Katika Hatua nyingine Nyota Huyo ameongeza kuwa Kuna maneno waliyoambiwa kabla ya Mchezo huo Kuanza “Walimu walituambia jamani mechi hi ya Historia hivyo Tupambane ili Tuingie kwenye vitabu vya Historia ”
Mshambuliaji Huyo Ameongeza kuwa kufunga na kutengeneza nafasi Ni Jambo la kawaida kwake “Yale matukio ya kufunga Mabao na kusababisha Mabao kwangu sio Jambo la ajabu nimekuwa nikiyafanya Toka kwenye ndondo na timu nyingine nilizowahi kucheza hivyo Ni Kama yamejiludia ” Ditram Nchimbi .
Katika Hali ya Utani na Furaha Ditram ameongeza kuwa “Watanzania tunajua Sema Basi TU tunashindwa kuaminika na tunakimbilia TU kulaumu Hawa wachezaji hawajitambui lakini je mmewaamini kabla ya maneno hayo Kuna “Mapro” Wanakuja mechi 30 hafungi akifunga makelele kibao Sisi Tunaweza bwana ” .
Upande wa Hali ya usalama kikosi hicho Kiko Nchimbi amewatoa hofu watanzania Kwani “Fujo ilikuwa ile TU ya kurusha maji uwanjani baada ya Kuingia vyumbani tulitoka na Kuingia kwenye gari na hakukuwa na Fujo yeyote kwa Sasa tuko Ethiopia tunasubiliaaa ndege ya kurejea Nyumbani Tanzania” alimalizia Ditram Nchimbi. Taifa Stars imefuzu michuano ya CHAN itakayofanyika nchini Cameroon mwaka 2020.