Sambaza....

Beki wa klabu ya Yanga, Vicent Andrew Dante ameugomea uongozi wa klabu ya Yanga kujiunga na kikosi cha Yanga kwa madai ya kutaka kulipwa kwanza fedha zake. Dante amedai kuwa Yondani na Abdul ambao walikuwa wamegoma pamoja wamepewa fedha kidogo ndio maana wamejiunga amehoji inakuwaje kwake inakuwa ni ngumu kulipwa hata kidogo? Dante amesema anachotaka yeye ni fedha tu.

Alipoulizwa Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Friedrick Mwakalebela kuhusu madai ya Dante amesema kamati tendaji ilikutana juzi na wamedhimia kumlipa madai yake iwapo fedha itakapopatikana. Mwakalebela amedai hali ya uchumi wa klabu kwa sasa sio nzuri walimuomba Dante arejee kikosini na kumuahidi watamlipa ila hakuwa tayari.

-Dante (kulia)

Mwakalebela alivyoulizwa kuhusu kuwalipa fedha kidogo Juma Abdul na Kelvin Yondani amesema klabu inadaiwa fedha za usajili na wachezaji wengi sio Dante pekee ake na wengine wameihama klabu kikubwa ni kuvumiliana tu wote watalipwa madai yao. Yondani na Abdul wamelipwa na baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga na sio klabu tutawalipa wote ambao wanatudai alidai Mwakalebela.

Sambaza....