Baada ya kuanza vibaya ligi kuu Tanzania bara kwa kufungwa goli 1-0 na Ruvu Shooting , timu ya soka ya Yanga imeenda kuweka kambi jijini Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Zesco .
Wakiwa jijini Mwanza , Yanga watacheza michezo miwili ya kirafiki, mchezo wa kwanza utakuwa dhidi ya Mbao Fc na mchezo wa pili utakuwa dhidi ya Pamba FC