Sambaza....

Mtandao wetu wa Kandanda tuliandika umuhimu wa wadau wa soka nchini kulisaidia shirikisho la soka nchini katika kukuza soka kwa vijana. Nia kubwa imeonekana kwa Shirikisho hili na ndio maana waliweza kuingia mkataba na Fountain Gate Academy ya Dodoma katika kuwatunza vijana ambao wanaonekana ni lulu kwa Soka la nchi hii. Wakati huo huo Shirikisho linaendelea kuendesha mashindano mbalimbali ya vijana nchini.

 

Katika kuonyesha umuhimu wa kuendelea kulijenga soka la vijana, klabu ya Munasa FC kutoka mjini Musoma wameweka kambi jijini Dar ikiwa ni ziara ya wiki moja ya kimichezo. Timu hii ni ya vijana wa chini ya umri wa miaka 20, na inaonekana ipo vizuri sana.

“Tumekuja Dar kwaajili ya ziara yenye lengo la kuwapa uzoefu zaidi wachezaji wetu” Nyerembe Munasa, Mkurugenzi wa timu hiyo aliuambia mtandao wa Kandanda.

Hawa U13, U15, U17 wakishamaliza mashindano wanaenda wapi?

Timu hiyo ambayo ipo chini ya Mkufunzi Juma Maswanya, imeshacheza mechi ya kirafiki na na timu ya kituo cha JMK Youth Park ya U20 na kufungwa bao 2-1. Kwa uchambuzi wetu Munasa walikuwa vizuri zaidi na kuonyesha wapo tayari kuwa kizazi cha soka hapo baadae na kuleta changamoto.

Uwekezaji ambao unafanywa na Mkurugenzi wa klabu hiyo bwana Munasa kwa mujibu wake unamalengo makubwa, ndio maana pia amemuhusisha mtalaamu wa soka la vijana Ticha Juma Maswanya.

Mwamko ni mkubwa sana kwa wadau na wawekezaji kuwekeza katika soka, lakini je ni kwa kipimo gani kuingiavkatika biashara hii na kufika ligi kuu muwekezaji anafaidika? Mtandao huu utakueletea maoni na mawazo yake na angalau kutoa majibu haya.

Sambaza....