Simba na Yanga wamejitoa katika mashindano ya Kagame Cup kwa sababu mbalimbali na kuifanya Tanzania iwe na mwakilishi mmoja tu ambaye ni Azam FC.
Azam FC itatuwakilisha katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika msimu ujao. Kama ilivyo kwa Azam FC, KMC FC nayo itatuwakilisba katika michuano hiyo ya shirikisho barani Afrika.
Kwa Azam FC siyo mara ya kwanza kushiriki michuano ya kimataifa, lakini kwa KMC FC ndiyo mara ya kwanza kushiriki michuano ya kimataifa ya Afrika.
Hawana uzoefu mkubwa na michuano hii ya kimataifa, na katika michuano ya Kagame Cup msimu huu kuna timu kubwa za kimataifa zitashiriki.
Msimu huu Kagame CUP itashirikisha timu kama As Vîta ya Congo ambao ni wana fainali wa kombe la shirikisho barani Afrka msimu juzi na msimu jana walifika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika kundi ambalo walikuwepo na Simba.
Pia michuano hii itakuwa na timu kama Zesco ya Zambia ambayo ilifika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika msimu huu.
Michuano hii itakuwa na nafasi kubwa kwa KMC FC kupata uzoefu wa michezo ya kimataifa. Uzoefu ambao hawakuwa nao awali.