Sambaza....

Kocha mkuu wa Biashara United amedai kuwa wanaenda kukutana na Simba ambayo ni bora kwa hiyo lazima tuwaheshimu.

“Simba ni timu bora wametoka kushiriki mashindano ya kimataifa na wamefanikiwa kwa asilimia 60. 70. Kwa hiyo wao ni bora”.

“Lazima tuwaheshimu tuwape heshima yao inayostahili”.

Lakini pamoja na kukiri kuwa Simba ni timu bora, kocha huyo ambaye tangu auchukue Biashara United amefanikiwa kutofungwa hata mchezo mmoja kwenye uwanja wa nyumbani amedai kuwa watapambana kupata matokeo mazuri.

“Tuna alama 33, tunahitaji alama 4 ili tufikishe alama 37 ambazo zitatuweka katika mazingira mazuri ya kutoshuka daraja, kwa hiyo nimewaandaa vijana wangu kwa ajili ya kupata alama tatu”

“Pamoja na kwamba Simba ni bora lakini nimewaandaa vijana wangu kisaikolojia ili kupata alama tatu katika mchezo huu”- alisema kocha huyo mkuu ambaye mwanzoni mwa msimu alikuwa Mbao FC.

Biashara na Simba wanakutana katika uwanja wa Karume mjini Musoma katika mkoa wa Mara huku Biashara ikishika nafasi ya pili kutoka mwisho na Simba ikishika nafasi ya pili kutoka mwanzo.

Sambaza....