Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa kamati yake ya Uchaguzi imetangaza Mei 5 kuwa siku ya uchaguzi wa Yanga.
Awali uchaguzi huo ulitangazwa kufanyika Aprili 28 lakini kutokana na siku hiyo itakuwa fainali ya michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Malangwe Mchungahela amesema kila kitu kitafanywa na Yanga wenyewe na wao watabaki kuwa wasimamizi pekee. “Uchaguzi wa Yanga utakuwa Mei 5 na kila kitu kitafanywa Yanga wenyewe sisi TFF tutakuwa waangalizi,” alisema Mchungahela.
Ratiba kamili ya uchaguzi wa Yanga.
- Aprili 2-7 Kuchukua fomu
- Aprili 9 Kikao cha mchujo kwa wagombea
- Aprili 10 kubandikwa kwa majina yaliyopitishwa
- Aprili 11-14 Pingamizi kwa wagombea
- Aprili 16-18 Kupitia pingamizi na usaili
- Aprili 18-23 Sekretariati kusikiliza maamuzi ya kamati ya maadili
- Aprili 24-26 Kukata rufaa
- Aprili 27-29 kusikiliza rufaa
- Aprili 30- Mei 4 Kampeni
- Mei 5 uchaguzi mkuu.