Sambaza....

Waliokuwa viongozi wa Yanga, Samuel Lukumay ambaye alikuwa Kaimu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, na Hussein Nyika ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili, kamati ya mashindano na mjumbe wa kamati tendaji wamejiuzulu leo.

Wote wawili wamejiuzulu ili kupisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ya Yanga. Akizungumza na waandishi wa habari, Samuel Lukumay kwenye ofisi za klabu hiyo.

Amedai kuwa amejiuzulu kwa ajili ya kupisha mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo tu. Hawajajiuzulu kisa kukwepa tuhuma za ubadhilifu zinazosemwa.

Wote kwa pamoja wamehakikisha kubaki kuwa wanachama wa Yanga wenye uwezo wa kugombea tena, na watakuwa wanatoa ushirikiano mzuri kwa klabu hii kipindi hiki ambacho wamejiuzulu.

Wote kwa pamoja wanajua timu yao kwa sasa inataka ubingwa wa ligi kuu na kombe la shirikisho, hivo wametoa ahadi ya kushirikiana na timu .

Pia wamewataka mashabiki wa Yanga kutoa ushirikiano mkubwa kwa timu ili kuhakikisha inatwaa ubingwa wa ligi kuu na ule wa kombe la shirikisho.

Pia wamewataka mashabiki wa Yanga kuendelea kuichangia klabu ya Yanga , ambapo mpaka sasa hivi michango imefika milioni 90.

Yanga inakabiriwa na mchezo wa robo fainali ya kombe la shirikiaho dhidi ya Alliance ya Mwanza utakaochezwa Mwanza Siku ya jumamosi ijayo. Timu itabaki chini ya baraza la udhamini.

Sambaza....