Sambaza....

Kocha mkuu wa Yanga , Mwinyi Zahera amedai kuwa kama Yanga ikiendelea hivi hivi hatoweza kuendelea nayo msimu ujao.

Kocha huyo ambaye alitoa wazo la wanachama kuichangia timu yao. Kocha huyo anaamini kuwa Yanga inaweza kujengwa na wana Yanga wenyewe.

Mwinyi Zahera anaamini kuwa dhana ya kuwa timu ya wananchi ni wana Yanga wao kushirikiana kuiendesha hii timu yao.

Lakini Mwinyi Zahera anashangaa kabisa jinsi ambavyo wana Yanga wanavyosua sua katika ujenzi wa timu yao.

Mwinyi Zahera ameendelea kusisitiza kuwa kama hali hii itaendelea hatoweza kuendelea kuwepo kwenye timu ambayo haina malengo.

Yeye hafuati timu yenye pesa, anafuata timu yenye malengo. Anaamini kabisa wana Yanga wenyewe wana nguvu ya kuitoa Yanga kutoka chini kwenda juu.

Mwinyi Zahera amedai kuwa hajawahi kusema Yanga itabeba kikombe chini ya mikono yake kwa sababu timu yake haina uwezo huo.

Hivo Yanga wanatakiwa wajisaidie wenyewe kwa kuchanga pesa ili msimu ujao waweze kujenga kikosi ambacho ni kipana kupitia michango ya Wananchi.

Sambaza....