Sambaza....

Njia ipi waliitumia Prisons kushambulia?

Walipokuwa katika robo yao ya uwanja walokuwa wanamiliki mpira kwa kupiga pasi huku wakispgea mbele.

Walipokuwa wanafika karibu na nusu ya uwanja walikuwa wanapiga mipira mirefu ya moja kwa moja kwa washambuliaji wao.

Walijua washambuliaji wao walikuwa na kasi kubwa sana ukilinganisha na mabeki wa Yanga , kasi hii iliwasumbua sana mabeki wa kati wa Yanga ( Dante na Cannavaro) katika kipindi cha kwanza.

Ndiyo maana hata goli la Prisons lilitokana na mpira mrefu uliopigwa moja kwa moja kwa washambuliaji wa Prisons ambao waliwazidi kasi mabeki wa kati wa Yanga na kufanikiwa kufunga.

Baada ya kadi nyekundu kutolewa kwao, aina yao ya ushambuliaji ilibadirika sana.

Kwani walianza kushambulia kwa kushtukiza tena kwa tahadhari huku wakijilinda.

Kadi nyekundu ilikuwa halali?

Ukiangalia dhamira ya mchezaji wa Prisons ilikuwa kufanya madhambi kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Yanga.

Mara nyingi, busara za mwamuzi huangalia dhamira ya mchezaji. Na dhamira ya mchezaji ilikuwa kumpiga kiwiko, kitu ambacho anastahili kupata adhau ya kadi nyekundu.

Prisons walikuwa wanazuiaje katika mchezo wa jana?

Wakati Prisons wakitumia mipira mirefu ya moja kwa moja kushambulia, wakati wa kuzuia walikuwa wanafanya kukaa na mchezaji kwa ukaribu ( man to man)

Hali ambayo iliwafanya Yanga wasiwe huru kupanga mipango yao ya kushambulia na kupata goli.

Kipi kiliwagharimu Yanga ?

Ukiachana na kwamba Prisons walikuwa wazuri sana katika kuzuia kwa kukaba man to man. Ila Yanga walikosa kiungo wa kati wa kusukuma timu.

Pato ngonyani, ni mchezaji mzuri hasa hasa linapokuja suala la yeye kutimiza majukumu ya kuzuia, lakini tatizo lake kubwa ni namna ambavyo anavyosukuma timu kwenda pele.

Pato alikuwa haifanyi/hailazimishi timu itembee mbele kwa kasi, hakuwa mtu wa mipango wa namna gani timu icheze.

Yanga walipokuwa wanazuia, viungo wa pembeni ( Emmanuel Martin na Pius Buswita ) walikuwa wanakuja katika kuongeza idadi ya viungo wa kati kuwa wanne. Hali hii iliwalazimu Prisons kutumia mipira mirefu kwa sababu ya wingi wa viungo wa Yanga waliokuwepo katikati hivo ikawa ngumu kwao kupitisha mipira kutumia eneo la katikati.

Lakini, Yanga walipokuwa wanashambulia eneo la katikati lilikuwa linabaki na watu wawili tu ( Raphael Daudi na Ibrahim Ajib ambaye alikuwa anashuka chini kidogo kumsaidia Raphael Daudi majukumu ya kuchezesha timu )

Kushuka kwa Ajib kuchezesha timu kulikuwa hakuna faida kwa Yanga kwa sababu Ajib jana alikuwa amekabwa sana.

Hivo Yanga walitakiwa, kuwafanya Emmanuel Martin na Pius Buswita kuwa wanakuja eneo la katikati kama ambavyo walivyokuwa wanashuka wakati wanashambuliwa.

Kwenda kwao pembeni hakukuwa na faida kwa sababu hawakuwa na madhara ya moja kwa moja kwa Prisons.

Hivo kuongeza kwao nguvu katika eneo la katikati kungewafanya Prisons waubane uwanja, kitu ambacho kingewapa nafasi Juma Abdul na Gadiel Michel kupitia pembeni. Kwa kasi yao kungesaidia kwao kupiga krosi zenye madhara.

Dante na Cannavaro walikuwa wanacheza man to man kwa wachezaji wa mbele wa Prisons.

Ukiwa unacheza man to man unatakiwa uwe makini na mijongee ya mpinzani wako.

Wakati goli la Prisons linapatikana,   Cannavaro alikuwa na mfungaji wa hilo goli, lakini alipozidiwa kasi ya mijongeo akamvisha mzigo mzito Dante .

Sambaza....